Home Kitaifa RAIS SAMIA AKUTANA NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI KUJADILI UWEKEZAJI

RAIS SAMIA AKUTANA NA KAIMU BALOZI WA MAREKANI KUJADILI UWEKEZAJI

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, amekutana na Kaimu Balozi wa Marekani, Andrew Lentz, Ikulu ya Chamwino kwa mazungumzo kuhusu kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi, kisiasa na kiusalama kati ya nchi hizo mbili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais – Ikulu, Shaaban Kissu, imeeleza kuwa mazungumzo hayo yapo katika hatua za mwisho za makubaliano ya miradi ya kimkakati ikiwemo LNG na Tembo Nickel, huku uchambuzi wa kiufundi wa Mradi wa Mahenge Graphite ukiendelea.

Marekani imeonyesha dhamira ya kukuza mahusiano ya kiuchumi yanayolenga manufaa ya pamoja, huku Rais Samia akiahidi kuharakisha taratibu za utekelezaji wa miradi hiyo. Taarifa hiyo imebainisha pia kuwa zaidi ya kampuni 400 za Marekani zinafanya shughuli za kibiashara nchini, ishara ya kuimarika kwa mazingira ya uwekezaji.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!