Home Kitaifa RAIS SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA 9 WA WAKUU WA MAJESHI

RAIS SAMIA AFUNGUA MKUTANO WA 9 WA WAKUU WA MAJESHI

Na Halima Hassan

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, leo Desemba 15, 2025 amewasili katika Shule ya Kijeshi ya Ulinzi wa Anga (SKUA), mkoani Tanga, kufungua rasmi Mkutano wa 9 wa Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Makamanda.

Mkutano huo unalenga kupitia utekelezaji wa majukumu ya Jeshi na kuweka mikakati ya kuimarisha ulinzi na usalama wa taifa.

Rais Samia anatarajiwa kutoa maelekezo mahsusi kuhusu ulinzi wa mipaka, amani, na ushiriki wa Jeshi katika maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Mkutano huu ni sehemu ya utaratibu wa kila mwaka wa JWTZ kujadili mafanikio, changamoto na mwelekeo wa ulinzi wa taifa.

Shughuli hiyo imehudhuriwa na viongozi waandamizi wa serikali, wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama, pamoja na makamanda kutoka maeneo mbalimbali nchini.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!