Charles Hilary Msemaji Mkuu wa serikali Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Mwinyi amemteua Charles Hilary kuwa Msemaji Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
Kabla ya uteuzi huo Charles Hilary alikuwa Mkurugenzi wa Idara ya Mawasiliano, Ikulu Zanzibar.
Uteuzi huo umeanza leo Februari 6, 2023.









