Home Kitaifa PPRA YAWAJENGEA UWEZO WAKUU WA VITENGO VYA UNUNUZI NCHINI,MATUMIZI YA MFUMO WA...

PPRA YAWAJENGEA UWEZO WAKUU WA VITENGO VYA UNUNUZI NCHINI,MATUMIZI YA MFUMO WA NeST.

Na Deborah Lemmubi -Dodoma.

MKURUGENZI wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) Bwana Denis Simba ameahidi kushirikiana na Mamlaka za Serikali za Mitaa katika kushughulikia changamoto zinazoukabili Mfumo huo wa ununuzi NeST hasa kwa wale wajanja wajanja wanaodhani mfumo huo hauna macho.

Bwana Simba amesema hayo Jijini Dodoma wakati akifungua Mafunzo ya matumizi ya Mfumo wa NeST kwa Wakurugenzi, Wataalam wa Tehama na Maofisa Ununuzi ngazi za Mikoa na Halmashauri.

Na kuwataka washiriki hao kuhakikisha michakato ya ununuzi wa miradi unaanzishwa haraka mara watakaporejea katika maeneo yao ya Kazi kwa zile Halmashauri ambazo zimekwisha kupata fedha za miradi.

Lakini niwahakikishieni hizi changamoto,wote tutashirikiana kuhakikisha kwamba tunazikabili na kuzitafutia suluhisho, hasa kwa wale wajanja wajanja ambao wanadhani mfumo huu hauna macho,kwasasa tupo tunakamilisha taratibu mbalimbali kuhakikisha kwamba mfumo wetu unakuwa imara na unakuwa suluhisho kwankutumia Tehama“.

Na nachukua fursa hii kuelekeza mkirudi kwenye maeneo yenu ya kazi mkahakikishe kuwa Halmashauri ambazo zimeshapokea fedha za miradi,michakato ya ununuzi wa miradi ikaanzishwe kwa haraka”.

Kwa upande wake Bwana Gilbert Kamnde ambaye ni Meneja wa kujenga uwezo na huduma za ushauri PPRA amesema washiriki hawa waliopata nafasi ya mafunzo haya wao ndio watakuwa machampioni na ndio watakaokwenda kuwezesha matumizi sahihi ya mfumo wa NeST na kuwasapoti wale watu wa ngazi za chini za Serikali,kama vile kwenye vituo vya afya,Zahanati, Shule za msingi,Shule za Sekondari,Kata mpaka kwenye ngazi ya vijiji kwasababu mfumo unafika mpaka kule na wanatakiwa kuutumia vizuri.

Lakini pia kwa wale watoa huduma katika ngazi za chini za Serikali pamoja na wazabuni katika ngazi zote kuanzia Halmashauri,Mkoa mpaka kwenye ngazi za chini za msingi wote wanatakiwa kutumia mfumo wa NeST ikiwemo wale ambao wanataka kufanya biashara na Serikali basi lazima watumie mfumo huo.

Naye mmoja wa washiriki kutoka Halmashauri ya Kondoa Bi Winfrida Mwabuke amesema kuwa wao wanaotoka kati ngazi za Halmashauri wana ngazi za vituo vya afya pamoja mashule, kwahiyo mfumo huu wa NeST umewasaidia kurahisisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwani kuna wakati walimu walitumia muda mwingi hata kupelekea kuacha vipindi na kwenda kutafuta wazabuni katika eneo lingine ili kupata vifaa,lakini kwa kutumia mfumo huu wa NeST Mwalimu hata akiwa shuleni anaweza kupata wazabuni kwa kutumia simu janja na kurahisisha shughuli zake zingine za ualimu.

Mafunzo haya yaliyoendeshwa na PPRA ni ya siku tatu ambayo yamelenga kuwajengea uwezo Wataalam wa ununuzi kutoka Halmashauri zote,Wakuu wa vitengo vya ununuzi, Maafisa ununuzi na ugavi,Wataalam wa Tehama na Wakuu wa vitengo vya ununuzi kutoka ofisi za Sekretarieti za Mikoa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!