Home Biashara PESAPAL YAWAHAKIKISHIA USALAMA NA ULINZI ZAIDI WATEJA WAO

PESAPAL YAWAHAKIKISHIA USALAMA NA ULINZI ZAIDI WATEJA WAO

PESAPAL imeboresha suluhisho lake la malipo ya biashara kidijitali (E-commerce) ili kuwezesha uthibitishaji wa miamala ya mtandaoni, teknolojia ya hali ya juu, utoaji wa taarifa na vipengele vya usalama vimeboreshwa

Akizungumza Jijini Dar es salaam Octoba 4 mwaka huu Mkurugenzi Mtendaji wa Pesapal, Agosta Liko amesema kutokana na ukuaji wa malipo ya biashara kidijitali kuongezeka Afrika Mashariki, Pesapal inaendelea kuwekeza katika teknolojia za kibunifu ili kuweka imani ya hali ya juu miongoni mwa watumiaji na wafanyabiashara.

“Kutokana na ukuaji wa hali ya juu kwenye biashara ya malipo kidijitali, imekuwa muhimu sana kipindi hiki kwa biashara zote kuwa na ulinzi thabiti na maboresho ya muonekano wa programu zao (API). Tumefurahishwa na aina mpya ya huduma inayotolewa kupitia Pesapal 3.0, na vipengele vipya vinatuwezesha kuleta huduma za ongezeko la thamani sokoni.”

Aidha Liko ameeleza kuwa kutokana na kukidhi viwango vya kimataifa vya malipo ya kielektroniki, wanaweza kukabiliana na hatari na hivyo kuongeza Imani kwa wateja katika matumizi ya kadi za mikopo na kadi za benki au hata fedha kwa njia ya simu katika mifumo ya malipo kidijitali (3DS) ni itifaki ya malipo iliyoundwa ili kutoa safu ya ziada ya ulinzi ili kusaidia kuzuia ulaghai kwa kuwawezesha watumiaji kujithibitisha kwa watoa kadi zao za malipo wanapofanya ununuzi kwenye chaneli za kidijitali.

Pia huwapa mawakala na watoa huduma njia ya uhakika ya kuthibitisha wamiliki wa kadi kwa miamala ya biashara kidijitali kabla ya kuwaidhinisha.

hata hivyo amevitaja Vipengele muhimu vya Pesapal kwa biashara na wateja ni pamoja na Uboreshaji wa muonekano wa program na uzoefu kwa mtumiaji

“Mchakato wa kulipa pesa kwa simu ya mkononi una programu na ulipaji wa hatua 2 endapo simu ya mteja haitumii kipengele hiki,Uchakataji salama wa kadi za malipo na mkopo kuhakikisha wateja na mawakala wanalindwa dhidi ya ulaghai.”

Pesapal imejitolea kutoa uzoefu wa malipo jumuishi na wa hali ya juu, kuhakikisha inatoa majibu yanayokidhi mahitaji ya kila siku ya wateja wake. Tangu 2009, Pesapal imeendelea kutoa Mazingira salama ya malipo huku ikizingatia viwango vya juu zaidi vya usalama.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!