Home Kitaifa NDC YATILIANA SAINI YA MIKATABA YA UCHIMBAJIA MAKAA YA MAWE NA MAKAMPUNI...

NDC YATILIANA SAINI YA MIKATABA YA UCHIMBAJIA MAKAA YA MAWE NA MAKAMPUNI MATANO YA WAZAWA

Na Magrethy Katengu

Serikali kupitia Shirika la Taifa la Maendeleo NDC limetiliana saini wa Mikataba ya Uchimbaji wa Makaa ya mawe katika mradi wa Mchuchuma na Wachimbaji Wazawa wa Makampuni matano yaliyoshinda Zabuni hiyo .

Waziri wa Viwanda na Biashara Dkt Ashatu Kijaji akishuhudia hafla ya utiaji saini Jijini Dar es salaam ameonyesha kufurahishwa na hatua hiyo iliyofikiwa huku akisema utiaji saini huo ni wa kihistoria katika miradi ya Liganga na Mchuchuma kwa kuwa ni uendelezaji wa Maono ya Awamu ya sita ya kuendeleza sekta ya Viwanda nchini.

”Hii ni dhamira ya dhati na ya hali ya juu ya seriakali ya awamu ya sita kuhakikisha ndoto za utekelezaji wa miradi ya Liganga na Mchuchuma sasa zinatimia na raslimali hizi ambazo zimekaa kwa muda mrefu bila kuwanufaisha wananchi ziwanufaishe na kuchangia katika uchumi wa nchi” amesisitiza Dkt Ashatu

Waziri Dkt. Ashatu amesema tayari Mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassani amekuwa mchango mkubwa. sana wa maendeleo kwani ameridhia kutoa kiasi cha shilingi bilion 15 .4 za kitanzania ikiwa ni malipo ya fidia ya wanufaika ambao watapisha utekelezaji wa mradi huo.

Awali akizungumza wakati akimkaribisha Mhe Waziri Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Maendeleo ( NDC) Dkt Nicholaus Shombe amebainisha kuwa awali mchakato huo ulihusisha jumla ya Kampuni 25 ambapo jumla ya Kampuni 17 zilifanikiwa kuwasilisha maombi yao kwa ajili ya uchambuzi na ushindani na zilipatikana Kampuni 5 zilizokidhi vigezo na vitalu hivyo vinakodishwa katika awamu ya kwanza ya mradi huo

”Kampubi 25 zilipewa nyaraka za Zabuni kupitia mfumo wa ununuzi Serikalini ( TANePS) ambapo Kampuni 17 zilifanikiwa kuwasilisha nyaraka za Zabuni” amesema Dkt Shombe

“Jumla ya Kampuni Tano zimetia saini makubaliano haya ya uchimbaji wa makaa ya uchimbaji katika Mradi wa Mchuchuma ambazo ni Sheby Mix investment Limited, Nipo Engineering Company Limited, Chusa Mining Company Limited , Kindain Company Limited, na Cleveland Mine and Service Company Limited Mkataba utakaodumu kwa miaka mitano” amesema Shombe

Naye Mkurugenzi. mwendeshaji wa Kampuni ya uchimbaji madini Mzawa kutoka Cleveland Mine and Services Company Limited Ndaisaba Ruhoro alisimama kwa niaba ya makampuni yote matano kutoa neno la. shukrani na kusema amempongeza Rais Dkt Samia. Suluhu Hassan kwa. kazi kubwa anayoifanya kufungua nchi kiuchumi kwani makaa ya Mawe hayo yanahitjika sana ndani na nje ya nchi hivyo imekuwa fursa kubwa kwa wazawa kupewa kipaumbele cha kupewa zabuni wanashukuru sana .

”Nina uhakika tumejipanga kukidhi vigezo tulivyopewa ili tuendelee kupewa fursa nyingine katika nchi yetu iliyobarikiwa raslimali za madini ya kutosha hivyo tutachimba kila mwezi tani elfu 30 tuna vifaa vya kutosha vya kufanyia kazi NDC mmetuamini na sisi hatutowaangusha” Amesema Ruhoro

Aidha Maradi huo utakuwa na. manufaa makubwa ya kiuchumi ikiwemo kutoa ajira zaidi ya miatano za moja kwa Moja kurahisisha upatikanaji wa nishati inayotokana na makaa ya mawe kwa viwanda jambo linalokwenda kuchochea ukuaji wa viwanda pamoja na. kuingiza fedha za kigeni.

Previous articleUN WOMEN yahamasisha Wanawake Pwani kugombea nafasi za uongozi katika chaguzi
Next articleBRELA yakutana na Taasisi za Udhibiti kuboresha mazingira ufanyaji biashara nchini

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here