Home Kitaifa MWANACHUO MORO AJARIBU KUJIUA NA KITU CHENYE NCHA KALI

MWANACHUO MORO AJARIBU KUJIUA NA KITU CHENYE NCHA KALI

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Waislamu Morogoro (MUM), Goodluck Charles Jactad (26), amenusurika kufa baada ya kujijeruhi vibaya kwa kujikata shingoni kwa kitu chenye ncha kali, katika jaribio la kujiua. Tukio hilo limetokea usiku wa Novemba 16, 2025, katika eneo la Msamvu, kata ya Mafisa, mkoani Morogoro.

Baada ya tukio hilo, mwanafunzi huyo alikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro kwa ajili ya matibabu na kwa sasa yupo chini ya ulinzi wa Jeshi la Polisi wakati uchunguzi wa kina ukiendelea ili kubaini chanzo halisi cha tukio hilo.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, SACP Alex Mkama, amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kueleza kuwa juhudi zinaendelea ili kujua mazingira yaliyompelekea kijana huyo kuchukua hatua hiyo hatarishi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!