


📌Waziri Kapinga akutana na wawekezaji wanaoatarajia kutekeleza mradi huo;
📌mradi kutekelezwa kwa awamu 6, kuanza kutekelezwa mwaka 2027
Na Neema Chalila Mbuja
Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe Judith Kapinga leo 22 Septemba,2026 amekutana na kufanya mazungumzo na wawekezaji wa kampuni ya SDIG ambao ndio wanaotarajia kutekeleza mradi wa makaa ya mawe ya mchuchuma na chuma cha Liganga.

Waziri Kapinga amesema kuwa utekelezaji wa mradi huo unatarajia kuanza rasmi mwaka 2027 na utatekelezwa kwa awamu sita ambapo kwa awamu ya kwanza utajumuisha mgodi wa makaa ya mawe, awamu ya pili ni mgodi wa chuma na ya tatu ni ujenzi wa kiwanda cha makaa maalumu ya kuyeyusha chuma kwa kutumia makaa ya mawe .
Awamu nyingine za ujenzi zitahusisha ujenzi wa kiwanda cha kuzalisha chuma, ujenzi wa kinu cha kuzalisha umeme kwa kutumia mvuke wa kiwanda kinachozalisha chuma na ujenzi wa barabara kilomita 70 kutoka mchuchuma hadi Liganga.
Aidha Mhe Kapinga amesema, utekelezaji wa mradi wa mchuchuma na liganga utaiwezesha Tanzania kufikia uchumi wa dola Trilioni moja ifikapo mwaka 2050.









