
Kwembe, Ubungo
Ziara ya kukagua maendeleo ya mradi utakaozinduliwa na Mwenge imefanyika katika Shule ya Sekondari Barbro Johanson iliyopo ndani ya Kata ya Kwembe. Mradi huo unahusisha ujenzi wa jengo la maktaba, chumba cha mitihani, hall la kujifunzia pamoja na maktaba ya kompyuta, wenye thamani ya shilingi bilioni tatu na milioni mia nane (3.8).

Ziara hiyo imefanyika tarehe 13/04/2026, ikiongozwa na Mheshimiwa Diwani wa Kata ya Kwembe, Kawina Hadji Konde, kwa lengo la kujionea hatua iliyofikiwa katika utekelezaji wa mradi huo na kuhakikisha unatekelezwa kwa viwango vinavyotakiwa ndani ya muda uliopangwa.
Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Diwani ameambatana na Kamati ya Mwenge ya Wilaya ya Ubungo, inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya, Mheshimiwa Albert Msando.








