Home Kitaifa MHANDISI LWAMO:MAPATO SEKTA YA MADINI YAPANDA KUTOKA ASILIMIA 7.2 MWAKA 2021 HADI...

MHANDISI LWAMO:MAPATO SEKTA YA MADINI YAPANDA KUTOKA ASILIMIA 7.2 MWAKA 2021 HADI ASILIMIA 9 KWA MWAKA 2023.

Na Deborah Lemmubi-Dodoma.

KATIBU Mtendaji wa Tume ya Madini Mhandisi Ramadhani Lwamo leo hii ameeleza kuwa makusanyo ya maduhuli ya Serikali yamepanda kutoka Shilingi bilioni 624.61 ikiwa ni makusanyo ya mwaka 2021/2022 hadi kufikia Shilingi bilioni 753.82 kwa mwaka 2023/2024.

Na pia Pato la Taifa katika sekta hiyo limeongezeka kutoka asilimia 7.2 mwaka 2021 hadi asilimia 9 mwaka 2023 iliyotokanq na uimarishwaji wa shughuli za madini.

Mhandisi Ramadhani ameyaeleza haya Jijini Dodoma Machi 4,2025 wakati akizungumza na Wanahabari akielezea mafanikio na utekelezaji wa Tume hiyo kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya wamu ya sita.

Kiwango cha makusanyo ya maduhuli ya Serikali kimepanda kutoka shilingi bilioni 624.61 zilizokusanywa mwaka wa fedha 2021/2022 hadi kufikia shilingi bilioni 753.82 mwaka wa fedha 2023/2024“.

Pia Mchango wa sekta ya madini kwenye Pato la Taifa umeongezeka kutoka asilimia 7.2 mwaka 2021 hadi asilimia 9 mwaka 2023 kutokana na kuimarika kwa usimamizi wa shughuli mbalimbali za madini”.

Aidha amesema ukuaji wa sekta ya madini umeongezeka kutoka asilimia 9.4 mwaka 2021 hadi kufikia asilimia 11.3 mwaka 2023 ambapo ukuaji wa sekta ya madini na mchango wake katika Pato la Taifa unatarajiwa kufikia asilimia 10 na zaidi ifikapo mwaka 2025.

Kwa upande mwingine amesema kuanzia mwaka wa fedha 2021/2022 mauzo ya madini katika masoko na vituo vya ununuzi wa madini yameendelea kuongezeka kutoka shilingi bilioni 2.361.80 hadi shilingi bilioni 2,597.18 kwa mwaka 2023/2024.

Suala la upatikanaji wa ajira kwa Watanzania amesema kuwa Tume hiyo imeendelea kusimamia kikamilifu upatikanaji wa ajira kwa Watanzania kwenye kampuni mbalimbali za uchimbaji wa madini.ambapo Ajira 19,874 zimezalishwa na makampuni ya uchimbaji wa madini ambapo kati
ya hizo, 19,371 ni Watanzania.

Mhandisi Lwamo amesema Tume imefanikiwa kutoa leseni 41,424 kati ya 37,318 zilizopangwa kutolewa katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya wamu ya sita ikiwa ni sawa na asilimia 111.

Tume imefanikiwa kutoa jumla ya leseni 41,424 kati ya 37,318 zilizopangwa kutolewa katika kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Sita ambayo ni sawa na asilimia 111. Leseni hizo zilijumuisha leseni za uchimbaji mkubwa, uchimbaji wa kati na uchimbaji mdogo“.

Sekta ya madini ni miongoni mwa sekta muhimu katika kukuza uchumi na kuleta maendeleo ya jamii na Taifa kwa ujumla.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!