Home Kitaifa MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA WAIMARISHA BEI ZA MAZAO MKOANI RUVUMA

MFUMO WA STAKABADHI ZA GHALA WAIMARISHA BEI ZA MAZAO MKOANI RUVUMA

Celebrating 25 Years of NHIF

Serikali imesema biashara ya mazao mkoani Ruvuma imeendelea kuimarika kupitia Mfumo wa Stakabadhi za Ghala unaosimamiwa na Bodi ya Usimamizi wa Stakabadhi za Ghala (WRRB), huku wakulima wakinufaika na bei nzuri ikilinganishwa na awali.

Hayo yameelezwa na Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga, alipokuwa akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika Songea mjini Novemba 10, 2026, wakati wa ziara ya Makamu wa Rais, Mhe. Deogratius Ndejembi, mkoani Ruvuma.

FAHARI AFYA

 Amesema mazao manne ya ufuta, korosho, mbaazi na choroko mkoani humo yanauzwa kupitia mfumo huo, hatua iliyosaidia kuboresha bei wanazopata wakulima.

Katika ziara hiyo, ambayo pia Mkurugenzi Mtendaji wa WRRB, Bw. Asangye Bangu ameshiriki, Makamu wa Rais ametembelea miradi ya hospitali na barabara katika Halmashauri ya Wilaya ya Mbinga na kuzungumza na wananchi katika mji wa Kigonsela.

Aidha, Makamu wa Rais ametembelea mradi wa maji katika Halmashauri ya Wilaya ya Madaba na kufanya mkutano wa hadhara Songea mjini, ambako amesisitiza umuhimu wa kusimamia vizuri miradi inayotekelezwa ili iweze kuwanufaisha wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!