Home Kitaifa MAHAKAMA YA KISUTU YAONDOA MAOMBI DHIDI YA GEOFFREY MMWAMBE NA VIONGOZI WA...

MAHAKAMA YA KISUTU YAONDOA MAOMBI DHIDI YA GEOFFREY MMWAMBE NA VIONGOZI WA ULINZI

Na Asella Denis

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es Salaam, leo Jumatatu Desemba 15, 2025, imeyaondoa rasmi maombi namba 289778/2025 yaliyokuwa yamefunguliwa Mahakamani hapo dhidi ya Waziri wa zamani Geoffrey Mmwambe, pamoja na viongozi wakuu wa vyombo vya ulinzi na sheria, akiwemo Mkaguzi Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP), Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini (DPP) na Mkuu wa Upelelezi Kanda Maalum ya Dar es Salaam (ZCO–DSM).

Uamuzi huo umetolewa na Hakimu Mkazi Gwantwa Mwankuga, baada ya Mahakama kukubaliana na hoja ya Wakili wa Serikali, Hekima Mwasipu, aliyeomba maombi hayo yaondolewe kwa sababu mlalamikaji alikuwa tayari ameshapatiwa dhamana tangu Alhamisi, Desemba 14, 2025. Hoja hiyo iliungwa mkono na upande wa Jamhuri.

Akizungumza na wanahabari Mahakamani hapo, Wakili Hekima Mwasipu amesema kuwa mteja wake anakabiliwa na makosa mawili; kosa la kwanza linahusu tuhuma za kupanga njama za kutaka kumuua Mkuu wa Jeshi la Polisi, huku kosa la pili likihusiana na tuhuma za uchochezi kupitia mitandao ya kijamii.

Ameongeza kuwa baada ya kupata dhamana jana, mteja wake alitakiwa kuripoti katika Kituo cha Polisi leo saa 3 asubuhi, ambapo alitimiza masharti hayo na kuachiwa. Aidha, upelelezi wa kesi hiyo unaendelea, na mteja anatakiwa kuripoti tena baada ya siku saba, kama inavyotakiwa kisheria.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!