Home Kitaifa MAADHIMISHO YA MWANAMKE DUNIANI ACB BENKI YAZINDUA WARIDI AKAUNTI

MAADHIMISHO YA MWANAMKE DUNIANI ACB BENKI YAZINDUA WARIDI AKAUNTI

Na Magrethy Katengu

Benki ya Akiba Commercial ikiwa Leo ni siku ya Maadhimisho ya mwanamke Duniani waja kivingine kuwasaidia Wanawake Wajasriamali kwa kuzindua akaunti ya WARIDI lengo ni kuwainua Wanawake wote wajasriamali hivyo wanashauriwa kujiunga benki hiyo.

Ushauri huo umetolewa leo Jijini Dar es salaam na Meneja Mwandamizi wa ACB Benki Magrethy Mwasumbi Wakati wa Uzinduzi wa Akaunti ya Wanawake ijulikanayo kama “Waridi” ambapo amesema akaunti hiyo imemlenga Mwanamke mjasriamali wa kitanzania anayepambana kuelekea safari ya mafanikio kwa maslahi Mapana ya jamiii inayomzunguka.

“Leo ni siku ya Maadhimisho ya Wanawake Duniani tumezindua akaunti ya Waridi hii Haina gharama za uendeeshaji za kila mwezi hakuna Makati ya kuchukua fedha kwa cashier,kuuliza salio ni bure na ujumbe mfupi yaani SMS Alert nayo ni bure“amesema Magrethy

Sanjari na hayo amesema Magrethy amebainisha mahitaji ya wateja huku kiu yetu ni akina mama kupatiwa bidhaa Maalumu kwa ajili yao ni wazo ambalo limeibuka hivi karibuni na bila kusita likafanyiwa kazi na leo inanekana fahari kuleta bidhaa mahusihusi kwa ajili yao

Hata hivyo amefafanua kuwa huduma hiyo ya akaunti ya wanaweka inazinduliwa Leo ni matokea ya mrejesho ya wateja pamoja na tafiti zetu kuhusia na viwango vya uridhikaji wa huduma zitolewazo sambamba na bidhaa.

Aidha wito unatolewa kwa Wanawake wote kujiunga na akaunti hii ya WARIDI kwani inafunguliwa na kwa shilingi za kitanzania na Dolla za Kimarekani popote pale mtu alipo atembelee matawi yaliyo karibu nao

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!