
Na Shomari Binda-Musoma
KATIBU wa Jumuiya ya Wanawake wa CCM Wilaya ya Musoma mjini Teddy Bageni amewahimiza wanawake kujiamini katika kipindi hiki cha kampeni.
Akizungumza na Mzawa Blog ofisini za jumuiya hiyo Teddy amesema kujimini kwenye kampeni kutawapa nafasi ya kumfikia kila mmoja kuomba kura.
Amesema wanachama wa CCM waliwaamini kwenye kura za maoni na kuwapa nafasi na kushinda na wanayo nafasi pia ya kushinda kwenye uchaguzi wa jumla.
Teddy amesema katika Wilaya ya Musoma mjini wapo wanawake waliosimama kuomba nafasi ya Mwenyekiti wa Mitaa na ujumbe na wana nafasi ya kushinda.
Amesema UWT Wilaya ya Musoma mjini kupitia viongozi wake kwa kushirikiana na wanachama wote watashiriki kampeni ya kuwaombea kura kwa wananchi.
Katibu huyo amesema wamejipanga vizuri katika siku 6 za kampeni kuomba kura na kuweza kufikia lengo