Home Biashara KAPINGA AELEZA MALENGO YA SEKTA YA VIWANDA KUFIKIA 2050

KAPINGA AELEZA MALENGO YA SEKTA YA VIWANDA KUFIKIA 2050

Celebrating 25 Years of NHIF

📌 Serikali inalenga kuongeza mchango wa sekta ya viwanda katika Pato la Taifa hadi kufikia asilimia 15 ndani ya miaka 25 ijayo.

📌 Zaidi ya asilimia 50 ya bidhaa zitakazouzwa nje ya nchi zinatarajiwa kuwa zimeongezwa thamani hapa nchini.

FAHARI AFYA

📌 Serikali inalenga kupunguza uagizaji wa bidhaa za kati kutoka Sh trilioni 24 mwaka 2024 hadi Sh trilioni 12 ndani ya miaka 10 ijayo.

📌 Viwanda vya kimkakati vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu vitaanzishwa, sambamba na kutengwa kwa maeneo maalumu ya kongani za viwanda.

📌 Ajira zinazotokana na viwanda zinalengwa kuongezeka kutoka asilimia 5.2 hadi asilimia 9, huku idadi ya wajasiriamali ikitarajiwa kufikia milioni 16 ndani ya miaka 10 ijayo.

DODOMA.

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith S. Kapinga, amesema Serikali inalenga kuongeza mchango wa sekta ya viwanda katika pato la taifa hadi kufikia asilimia 15 ndani ya miaka 25 ijayo, ikiwa ni sehemu ya mikakati ya kukuza uchumi na kuimarisha uzalishaji wa bidhaa nchini.

Akizungumza Novemba 2, 2026, Bungeni jijini Dodoma, wakati akijibu na kuchangia hoja zilizotolewa na wabunge kuhusu mpango wa maendeleo, Kapinga amesema Serikali imepokea maoni yao kwa moyo wa dhati kwa kuwa yanaendana na mipango ya kuboresha sekta ya viwanda na biashara.

Amesema pamoja na kuongeza mchango wa viwanda katika pato la taifa, ikiwalengo ni kuhakikisha kuwa ndani ya miaka 25 ijayo, zaidi ya asilimia 50 ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi zinakuwa zimeongezwa thamani hapa nchini, badala ya kuuza malighafi bila kuzichakata.

Katika eneo la masoko, Kapinga amesema Serikali inalenga kuongeza mauzo ya bidhaa zinazozalishwa nchini na kupunguza uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi, akibainisha kuwa mwaka 2024 Tanzania iliagiza bidhaa za kati zenye thamani ya Sh trilioni 24, ndani ya miaka 10 ijayo watakuwa wakiagiza bidhaa za Sh. trilioni 12, hatua itakayosaidia kupunguza utegemezi wa bidhaa kutoka nje.

Aidha, Kapinga amesema matarajio hayo yanaendana na Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050, ndiyo maana sekta hiyo imefanya tathmini na kuona umuhimu wa kuwa na Sera mpya ya Maendeleo Endelevu itakayokwenda sambamba na mipango ya sasa ya maendeleo, amesema Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mwigulu Nchemba, anatarajiwa kuzindua sera hiyo Novemba 4, 2026, Jijini Dodoma.

Vilevile, Mhe. Kapinga amesema Serikali imejipanga kuanzisha viwanda vya kimkakati vinavyotumia teknolojia ya hali ya juu, pamoja na kutenga maeneo maalumu kwa ajili ya kongani za viwanda na shughuli za ubunifu zitakazochochea ukuaji wa uchumi na kuongeza ajira nchini.

Amesema katika kipindi cha miaka 10 ijayo, Serikali inalenga kuongeza ajira zinazozalishwa na viwanda kutoka asilimia 5.2 hadi asilimia 9, huku ikiweka mkazo katika kukuza biashara changa na ubunifu kupitia kitengo maalumu cha intelijensia ya masoko na ubunifu kilichoanzishwa ndani ya Wizara.

Aidha, amesema kupitia mapitio ya Sera ya Maendeleo ya Jasiriamali ndogo na za Kati ya mwaka 2003, ni kuongeza idadi ya wajasiriamali kutoka milioni 6 hadi milioni 16 na kuongeza ajira zinazotokana na sekta hiyo kutoka milioni 11 hadi milioni 36 ndani ya miaka 10 ijayo kuelekea mwaka 2050.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!