Home Biashara KAPINGA AWAASA WANAFUNZI KUZINGATIA MASOMO, KUEPUKA VISHAWISHI

KAPINGA AWAASA WANAFUNZI KUZINGATIA MASOMO, KUEPUKA VISHAWISHI

Celebrating 25 Years of NHIF

Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb), amewahimiza wanafunzi kuzingatia masomo, kuepuka vishawishi na kutumia vyema muda wao wa masomo kujijengea maarifa yatakayowasaidia katika maisha yao ya sasa na baadaye.

Waziri Kapinga ametoa rai hiyo Novemba 2, 2026, jijini Dodoma, wakati wa uzinduzi wa Maonesho ya Bidhaa na Huduma za Viwanda na Biashara sambamba na Huduma za Kliniki za Biashara, yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete (JKCC), ambapo alizungumza na wanafunzi wa Chuo cha Biashara (CBE) waliohudhuria hafla hiyo.

FAHARI AFYA

Amesema elimu ni msingi muhimu katika maisha ya mwanadamu kwa kuwa humwezesha mtu kupata maarifa na ujuzi unaomsaidia katika nyanja mbalimbali, badala ya kuichukulia kama njia ya kupata ajira pekee.

Ameeleza kuwa wanafunzi wanapotembelea maonesho na kujifunza kuhusu shughuli mbalimbali za kiuchumi, wanapata maarifa ya ziada yanayoweza kuwasaidia katika maisha yao ya kila siku.

Aidha, amewashauri wanafunzi kuweka kipaumbele katika masomo yao wanapokuwa shuleni, akisisitiza kuwa kila jambo lina wakati wake, hivyo wanapaswa kuepuka vishawishi vinavyoweza kuwatoa kwenye malengo yao ya kitaaluma.

Amewasisitiza kusoma kwa bidii na kufanya vizuri katika mitihani yao ili kutimiza ndoto zao na kuwafanya wazazi na walezi wao wajivunie mafanikio yao, akitambua kuwa wazazi wamekuwa wakijitoa na kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika elimu ya watoto wao.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!