Home Kitaifa JWT KAGERA WAIOMBA SERIKALI KUENDELEA KUZITATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAFANYA BIASHARA

JWT KAGERA WAIOMBA SERIKALI KUENDELEA KUZITATUA CHANGAMOTO ZINAZOWAKABILI WAFANYA BIASHARA

Na Theophilida Felician Kagera.

Jumuiya ya wafanyabiashara Mkoa Kagera (JWT) imeiomba Serikali kuendelea kuzifanyia kazi ya utatuzi kwa baadhi ya changamoto kadhaa zinazowakabili wafanyabiashara wa wamaeneo mbalimbali ya Mkoa.

Aliyaomba hayo Mwenyekiti wa jumuiya hiyo Mkoa Kagera Nicholaus Jovin kwenye mkutano wa waandishi wa habari ofisini kwake Manispaa ya Bukoba awali ameanza kwakuishukuru Serikali ya Mkoa kwa namna ambavyo imekuwa ikichukua hatua madhubuti ya kuzitatua kero za wafanyabiashara kwa malengo ya kuwawezesha kufanya biashara zao katika mazingira rafiki yasiyokuwa na bughudha .

Tunashukuru Serikali chini ya Mkuu wa Mkoa wetu Albert Chalamila mara zote imekuwa ikichukua kero na changamoto zinazotolewa na wafanyabiashara na kuzitafutia ufumbuzi yapo mambo mbalimbali yanayopatiwa ufumbuzi baada ya kuyawasilisha kwa viongozi wetu wa Serikali” amesema Mwenyekiti Nicholaus Jovin

Ameendelea kueleza kuwa wao kama JWT wameshuhudia Serikali ya Mkoa ikiendelea kujenga mazingira yakuvutia shughuli za uwekezaji katika Mkoa jambo ambalo ni zuri na litakuwa chachu yakuinua kiwango cha uchumi.

Nicholaus pia amefafanua kuwa licha ya jitihada hizo bado kuna changamoto za hapa na pale zinazojitokeza kwa wafanya biashara hivyo kuathiri shughuli za biashara ambapo baadhi ya changamoto na kero tayari jumuiya hiyo imeziwasilisha katika ngazi mbalimbali kwa ajili ya kupatiwa ufumbuzi.

Ameongeza kwamba licha ya baadhi ya changamoto kupatiwa ufumbuzi bado zimekuwa zikiibuka tena hali inayosababisha kukosekana kwa utulivu wa kibiashara, utulivu wa kibiashara unapokosekana unaathiri mambo mengi ikiwa ni pamoja na kudhoofisha mitaji ya wafanyabiashara pamoja na mzunguko wa fedha.

Moja ya changamoto hizo ameitaja kuwa ni pamoja na baadhi ya wafanya biashara kuandikiwa barua za kutakiwa kulipa madeni ambayo yalishatolewa maelekezo na viongozi wa Serikali ngazi za juu.

“Mhe Rais Dr Samia Suluhu Hassani mwaka jana alipokuwa Mkoani hapa Kagera alipokea kilio cha wafanyabiashara juu yakudaiwa madeni ya kodi za miaka 5 nyuma na kuendelea baada yakuzingatia changamoto mbalimbali zilizowasilishwa kwake aliziagiza mamlaka husika madeni hayo yasidaiwe cha ajabu baadhi yawafanya biashara mpaka sasa wameendelea kudaiwa madeni hayo mpaka ya mwaka 2014 hali ambayo ni yaukiukwaji mkubwa wa maelekezo ya Mhe Rais tumepokea malalamiko sana hapa ofisini hivyo tunaziomba mamlaka husika kusitisha utaratibu huo kwani ni kinyume na maelekezo ya Mhe Rais Dr Samia na hali hii ikiendelea itaondoa utulivu wa kibiashara” amesisitiza Nicholaus Jovin.

Hata hivyo amehitimisha akisema kuwa kero na changamoto hizo ni muhimu kupata ufumbuzi wa kudumu kwakuwa zinakata mitaji ya wafanya biashara na kuathiri uwezo wakulipa mapato mbalimbali ya Serikali ambayo yanatengwa kutumiwa na Serikali kwa ajili ya ujenzi wa maendeleo ya wananchi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!