Na Magrethy Katengu
Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la hifadhi ya Mazingira (NEMC )wameandaa kongamano la kitaifa litakalohusisha viongozi wa Dini zote kujadiliana kwa pamoja kuhusu Sauti katika nyumba za ibada.
Akizungumza na Waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tanzania (JMAT) na kamati za amanin Nchini Sheikh Dkt Alhad Mussa Salum amesema Kongamano hilo viongozi wa dini na Madhebu yote wanatakiwa kuhudhuria na litaongozwa na kauli mbiu isemayo “Kongamano la kujenga uelewa kuhusu athari zitokanazo na sauti zilizozidi viwango katika nyumba za ibada ” hivyo ni fursa ya kutoa uelewa siku hiyo badala ya kuwa na minong’ono au kugombana.
“Niwasisitize sana kuhudhuria kwani kutakuwa na mada mbambali za kutujenga ikiwemo, utiifu wa mamlaka kwa mujibu wa Biblia Takatifu na Qur’an tukufu, uchungaji wa haki za wengine kwa mujibu wa Qur’an na Biblia Takatifu, sheria ya Mazingira ya 2004 na kanuni zake, athari zitikanazo na sauti zilizozidi viwango, usimamizi wa mipango miji, uelewa wa usajili wa asasi za kiraia , majukumu na wajibu Rita kwa taasisi za kidini” amesema Sheikh Dkt Alhad
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Baraza la Taifa la hifadhi ya Mazingira NEMC Dkt Stanley Gwamaka siku hiyo itakuwa ya kipekee sana viongozi wa dini watapata elimi ya kutosha namna ibada zao wanazoendesha sauti zisilete athari kwa wengine kila mmoja atatoka akiwa amefundishwa kwa kutumi kiabu chake anachokiamini na wao watakuwa mabalozi Waziri kwa wengine .
“Tunatoa elimu hii kwa ajili ya uelewa kila mtu afahamu hata kama yupo katika furaha au huzuni kiasi gani kuna kiwango cha sauti hatakiwi kuvuka na akivuka analeta athari za kifya kwa wengine” amesema Mkurugenzi Gwamaka
Aidha Kongamano hilo linatarajiwa kufanyika June 12 mwaka huu katika ukumbi wa Julius Nyerere International Convention(JNICC) kuanzia saa 3 asubuhi mpaka saa 11 jioni na Mgeni rasmi atakuwa Waziri Mkuu Mh Majaliwa Kasim Majaliwa litajenga uelewa utkaofikishwa kwa waumini wote kuishi kwa amani na utulivu.








