Home Kitaifa JESHI LA POLISI LATOA TAARIFA KUHUSU HALI YA USALAMA NCHINI

JESHI LA POLISI LATOA TAARIFA KUHUSU HALI YA USALAMA NCHINI

Na Halima Issa Hassan

Jeshi la Polisi Tanzania limesema kuwa hali ya usalama nchini imeendelea kuimarika, hususan katika kipindi cha usiku, kutokana na ushirikiano kati ya jeshi hilo, vyombo vingine vya ulinzi na wananchi.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Msemaji wa Jeshi la Polisi kutoka Makao Makuu ya Polisi jijini Dodoma, imeelezwa kuwa hadi kufikia saa 6 usiku, hali imeendelea kuwa shwari katika maeneo mbalimbali ya nchi. Hali hiyo imeelezwa kuwa ni miongoni mwa mafanikio ya juhudi za pamoja katika kuimarisha doria na ulinzi.

Aidha, jeshi hilo limewahakikishia wananchi kuwa mikakati ya kuendeleza ulinzi na kudumisha amani itaendelea kutekelezwa bila kusita, lengo likiwa kuhakikisha usalama wa maisha ya watu pamoja na mali zao.

Taarifa hiyo pia imeeleza kuwa mawasiliano na ushirikiano baina ya wananchi na vyombo vya usalama yataendelea kuhamasishwa ili kusaidia kufichua uhalifu na kuwezesha taifa kuendelea kuwa na amani na utulivu.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!