Pichani Mkurugenzi wa Kozi za Shahada na zisizokuwa za Shahada wa Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha( RUCU) Dkt Wille Migodela (wakatikati) akifuatilia maelekezo yanaoyotolewa na mmoja wa maafisa wa udahili wa Chuo hicho Kwa mwanafunzi aliyetembelea banda lao la maonyesho ya 17 ya Tume ya Vyuo Vikuu Nchini( TCU), jijini Dar es salaam.
Na Magrethy Katengu
Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha (RUCU) ili katika kuhakikisha changamoto zinazoikabili Jamii zinapatiwa ufumbuzi kimeamua kimejikita kutoa Elimu kwa wanafunzi kwa kivitendo zaidi kufanya ubunifu wa tafiti mbalimbali ili kusaidia kuleta suluhisho ya matatizo ya kimazingira yanayolikumba Taifa ikiwemo Ugonjwa wa Malaria ambao umekuwa tishio barani Afrika.
Akizungumza na Waandishi wa habari Dar es salaam Mkurugenzi wa kozi za Shahada na zisizo za Shahada Chuo Kikuu cha Katoliki Ruaha(RUCU) Dkt Wille Migodela katika Maonyesho ya ya 17 ya Elimu ya juu yaliyoandaliwa na Wizara ya Elimu Sayansi na teknolojia kupitia Time ya Vyuo Vikuu nchini (TCU) katika Viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es salaam ambapo amesema wanafunzi hao pia wanafanya tafiti juu ya magonjwa mengine ya ngozi( Fangasi) na kikohozi kupitia mimea ya asili kwa kutengeneza dawa .
Hata hivyo amesema chuo hicho wanafunzi wanaojiunga hapo hawaangalii dini wanawapokea wote na kuwapa uhuru wa kuabudu katika kulingana na Imani zao hivyo wanahakikisha program za Kozi mbalimbali wanazozitoa zinakuwa tofauti na Vyuo vingine na zinajikita katika utafiti wa Ubunifu huku zikipewa kipaumbele ili kumsaidia mwanafunzi anaehitimu kuondokana na zana ya kutemea kuajiriwa na badala yake aweze kujiajiri wenyewe.
” Wanafunzi wetu tayari wamefanikiwa kubuni kifaa cha kufukuza Mbu anayesababisha malaria kikifungwa ndani Mbu wote ndani ya nyumba wanamkimbia hivyo tayari tumeshakifanyia majaribio chuoni na kukitumia “amesema Dkt Wille
Sambamba na hayo amesema Wanafunzi wamebuni kifaa kinachopima uzito wa mizigo inayobebwa na magari ambapo kifaa hicho kinafungwa kwenye gari na gari hiyo haitapita kwenye mzani kwa ajili ya kupimwa, badala yake kifaa hicho kitaonyesha ukomo wa uzito kamili unaohotajika wakati kupakia mzigo Kwa kuwaka taa nyekundu au kutoa mlio .
“Magari yanatumia muda mrefu kukaa kwenye foleni ya mzani kupima uzito wa mzigo, wakati mwingine kufanya njia za udanganyifu wanapovuka mizania kupakia mizigo mingine hivyo sisi kama RUCU tumekuja na suluhisho la kubuni kifaa cha kisayansi kitakachoonyesha ukomo wa uzito wa mzigo unaotakiwa kupakiwa” amesema Dkt Migodela
Aidha pia amesema pia wamebuni mashine ya kupimia juisi kulingana na uhitaji wa mteja hivyo wazazi,walezi wanakaribishwa kuleta wanafunzi katika chuo hicho kwa mwaka huu wa masomo 2022/ 2023 wanatarajia kudahili wanafunzi wapatao 1400 ambapo wanafunzi wa cheti na Diploma ni 700 na wengine 700 ni Shahada(Digree),ambapo amesisitiza kwamba mazingira ya kujisomea kwa wanafunzi ni mazuri na gharama ni nafuu.