Home Biashara APONGEZA JITIHADA ZA WIPO KUENDELEZA UBUNIFU

APONGEZA JITIHADA ZA WIPO KUENDELEZA UBUNIFU

Afisa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Usajili wa Biashara na Leseni (BRELA), Bw. Godfrey Nyaisa amepongeza Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO) kwa jitihada linazozifanya za kuendeleza kazi za ubunifu kwa maendeleo ya nchi wanachama.

Pongezi hizo amezitoa wakati akiwasilisha taarifa ya nchi kuhusu Miliki Ubunifu na ushirikiano kati ya Tanzania na WIPO katika Mkutano Mkuu wa 63 wa Shirika la Miliki Ubunifu Duniani (WIPO), unaofanyika Geneva Uswisi.

Bw. Nyaisa amesema jitihada hizo za kuendeleza kazi za ubunifu kwa maendeleo ya nchi wanachama, zitazaa matunda na kuendeleza bunifu mbambali na kuleta tija kwa nchi wanachama.

Ameeleza pia ushirikiano kati ya Tanzania na WIPO utalenga katika kusaidia wajasiriamali na vijana katika kutumia Miliki Ubunifu kwa maendeleo ya ubunifu.

Mkutano huo wa siku saba ulioanza tarehe 14 Julai, 2022, unahudhuriwa pia na Mkurugenzi Mtendaji wa Wakala wa Usajili wa Bishara na Mali, (BPRA) Zanzibar, Bi. Mariam Mliwa Jecha, Mkuu wa Idara ya Uraghbishi wa Ushindani kutoka Tume ya Ushindani (FCC) Bi. Magdalena Utouh pamoja na Msajili Msaidizi Mkuu kutoka BRELA, Bi. Loy Mhando.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!