Baraza kuu la Waislamu wa Tanzania ( Bakwata ) Mkoa wa Mwanza, limefanya maandamano ya amani kupinga mapenzi ya jinsia moja, Ushoga, ulawiti, ukatili wa kijinsia pamoja na mauaji.

Aidha Bakwata Mkoa wa Mwanza, wamesema wamepokea na kuunga mkono hotuba ya Mheshimiwa Muft na Sheikh Mkuu wa Tanzania Sheikh Dkt, Abubakari Zuber Bin Ally juu ya kupinga na kukemea vikali matendo yote haramu

Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Hassan Kabeke ameishukuru Serikali kwa umakini wake wa kuchukua hatua za haraka pale tu inapobaini kuwepo na ulazima wa kupiga marufuku kuendelea kutumika kwa vitabu visivyo faa katika shule zetu nchini

Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislam Tanzania ( Bakwata ) Alhaji Nuhu Jabir Mruma amelipongeza Baraza Kuu la Waislam Mkoa wa Mwanza kwa kuunga mkono hotuba ya Mheshimiwa Muft na Sheikh Mkuu wa Tanzania Dkt, Abubakar Zuber Bin Ally juu ya kupinga na kukemea vikali viendo vyote haramu.









