Home Kitaifa ASKARI WAKIKE POLISI, JWTZ, MAGEREZA, UHAMIAJI, ZIMAMOTO NA UOKOAJI WATEMBELEA KITUO CHA...

ASKARI WAKIKE POLISI, JWTZ, MAGEREZA, UHAMIAJI, ZIMAMOTO NA UOKOAJI WATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA NTOMA

Na Theophilida Felician Kagera.

Askari wa kike kutoka jeshi la Polisi dawati la jinsia pamaja na askari wengine kutoka majeshi mengine ambayo ni Jeshi la wananchi JWTZ, Uhamiaji, Magereza pamoja na Jeshi la zima Moto na uokoaji Mkoani Kagera wameungana pamoja nakufanya ziara ya kukitembelea kituo cha kulelea watoto yatima Ntoma kilichopo kata ya Kanyangereko Halmashauri ya Bukoba.

Askari hao wakiongozwa naye Mkaguzi msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa Kagera Suzani Kamwaga wametoa zawadi za vitu mbalimbali vyakuwasaidia watoto ikiwemo mchele, sabuni, mafuta yakupikia naya kujipaka, sukari, na maji.

Suzani akizungumza kabla ya kukabidhi vitu hivyo amesema kuwa wameamua kuwatembelea watoto hao kwani Jeshi hilo kitengo cha dawati la jinsia pia limekuwa ni sehemu ya kuwapeleka watoto katika kituo hicho “haya ni moja ya majukumu yetu yakufanya kazi na jamii hasa watoto sababu kama kituo hiki sisi tumekuwa ni sehemu ya kuleta watoto hapa watoto ambao tumekuwa tukiwaleta hapa wengine ni waliotupwa na wengine kutelekezwa kwahiyo katika majukumu yetu ya kazi kama dawati la jinsia tumekuwa tukiwaleta katika kituo hiki”amesema Suzani Kamwaga.

Ameendelea kusema kuwa wamefanya hivyo ndani ya kipindi cha kilele cha maadhimisho ya sikukuu ya wanawake Duniani “sisi pamoja yakuwa watu wa majeshi lakini pia ni mama, ni walezi tunazaa tunauchungu na watoto na katika mazingira tunayowaokota yanakuwa ni mazingira magumu ni watoto wenye uhitaji wengine hawana msaada kabisa sasa kwa umoja wetu tumekusanya vitu kwa matumizi ya kufua nguo na chakula” ameongeza Suzani Kamwaga.

Askari Zusani akiambatana na wenzake ameingia katika vyumba wanamoishi watoto ili kijionea hali ya maendeleo yao ambapo kaimu wakituo Annamelis amemweleza kuwa baadhi ya watoto wanaolelewa hapo wameokotwa baada ya kutupwa wengine mama zao wamefariki kutokana na sababu mbalimbali.

Blandina Stephen mwakilishi wa Jeshi la wananchi (JWTZ) amebainisha kuwa katika kuazimisha sikukuu ya wanawake wao kama wanawake wanajeshi wameguswa pakubwa na kuamua kuungana pamoja na wanawake wa majeshi mengine katika kuwafikia watoto wakituo hicho ili waweze kuwafariji ukizingatia ni watoto ambao wamefikishwa hapo kutokea katika mazingira magumu.

Kaimu wa kituo hicho Anamelis kashasha akitoa taarifa fupi kwa askali hao amesema kituo hicho kilianzishwa mwaka (1952) kinapokea watoto yatima na wengine waliotelekezwa kwa sasa kina jumla ya watoto 35 japo uwezo wake ni wakutunza watoto 30 tuu, hivyo ametoa shukrani kwa askali hao kwanamna walivyowiwa nakukifikia kituo hicho.

Hata hivyo Askari wote kwa pamoja wamewafariji watoto kwa namna tofauti tofauti ikiwemo ya kuwabeba sambamba na kuwapakata mikononi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!