Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan na Viongozi wengine akiwa kwenye maandamano ya Kitaaluma wakati walipokuwa wakiingia kwenye Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu kwa ajili ya kushiriki Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) ambapo Chuo hicho kimemtunuku Shahada ya Heshima ya Uzamivu kwa kutambua mchango wake wa kuifungua nchi kiuchumi kupitia Sekta ya Utalii tarehe 28 Desemba, 2023.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, akizungumza na Rais Mstaafu wa Zanzibar Mhe. Dkt. Aman Abeid Karume katika Ukumbi wa Dkt. Ali Mohamed Shein Kampasi ya Tunguu walipohudhuria Hafla ya Mahafali ya 19 ya Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) tarehe 28 Desemba, 2023.
Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Uzamivu ya Usimamizi wa Utalii na Masoko yaani Doctor of Philosophy in Tourism Management and Marketing (Honoris Causa)
Shahada hiyo ametunikiwa na Chuo Kikuu cha Taifa Cha Zanzibar (SUZA)
“Nimekubali shahada hii ya Heshima ya Uzamivu ya Usimamizi wa Utalii na Masoko, Jukumu hili nitalitekeleza“ Rais Dkt. Samia