Shirika la Viwango Tanzania (TBS ) Juni 9 limesaini mkataba wa ushirikiano baina yake na Tamisemi kwa Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Mwanza ili kurasimisha zoezi la utekelezaji wa Kanuni ya ushirikiano,ya mwaka 2021.
Katika ngazi za Halmashauri kwa kuzingatia Sheria ya Viwango sura 130 pamoja na Sheria ya Fedha ya mwaka 2019 na kanunu zake za mwaka 2021.

Katika zoezi hilo la utiaji saini Katibu Tawala wa Mkoa wa Mwanza Elkana Balandya ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo,akawataka Wakurugenzi wa Halmashauri za mkoa huo kuhakikisha wanazingatia kwa umakini na kwa kutumia utaalamu kuhusiana na majukumu yaliyoshirikishwa kwenye majukumu ya udhibiti ubora wa bidha za chakula na vipodozi,
“Ninaamini kuwa tukizingatia matumizi sahihi ya Kanuni ya Mashirikiano kama ambavyo imewaairishwa na TBS itakuwa njia muafaka ya kuleta tija zaidi katika juhudi za kuleta maendeleo katika udhibiti wa bidha za chakula na vipodozi katika mkoa wete na Taifa kwa ujumla”
Aidha Balandya ametoa wito kwa watumishi wa serikali kuwa majukumu waliyopewa yakawe chachu ya kutumikia umma kwa bidii bila ubaguzi, kuwashauri na kuwasaidia kitaalamu pale itakapohitajika ili bidhaa ziwe na bora na salama na uchumi uendelehe kukua
Katika hafla hiyo ya utiaji saini pia TBS imeweza kutoa vitendea kazi cha kuanzia majukumu hayo ambacho ni ” kishikwambi kimoja kwa kila Halmashauri ya Wilaya ambapo alisisitiza kitendea kazi hicho kutumika kwa majukumu ya udhibiti ubora na usalama wa bidhaa za chakula na vipodozi na kutunzwa katika hali ya usafi na salama.

Mwenyekiti wa Halmashauri ya Ukerewe Joshua Manumbu amesema uamuzi huo utasaidia kutatua changamoto kwa wananchi ya kutumia vyakula na vipodozi visivuokidhi Viwango huku akisema katika eneo la Ukerewe udhibiti umekuwa mgumu kutokana na watumishi wa TBS kuwa wachache hivyo kwa kugatua madaraka hayo na kuyapeleka katikangazi za Halmashauri pamoja na kuwa na mratibu mmoja kwa uahirikiano wa Halmashauri wataweza kupunguza tatizo hilo ata kama lisipomalizika.
“Baada ya kuwa tumekasimisha majukumu kwa Halmashauri tunatarajia kwamba afya za wananchi ambao ndio walaji au watumiaji wa vipodozi au walaji katika migahawa,baa watakuwa sasa wana uhakika kwamba bidhaa zimeweza kuangaliwa katika maeneo hayo yanayotoa huduma yameweza kukaguliwa yamekidhi matakwa ya Viwango na vigezo vya kuwa baa au hotel kwa maana hiyo watakuwa salama zaidi” Happy Brown, Meneja wa TBS Kanda ya Ziwa.
Hafla hiyo hiyo ya utiaji saini imehudhuliwa na Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri za Jiji, Manispaa na Wilaya za mkoa wa Mwanza, Mstahiki Meya wa Jiji na Manispaa na Wenyeviti wa Halmashauri za Wilaya za mkoa wa Mwanza na watumishi wa TBS Kanda ya Ziwa.








