Na Magrethy Katengu
Serikali kupitia shirika la Reli Tanzania imesema reli ya Treni ya Umeme (SGR) ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 98 na baadhi ya mabehewa yameshafilka tayari kuanza safari ya kuanzia Dar ea salaam mpaka Morogoro zinatarajiwa kuanza mwezi Julay mwaka huu
Akizungumza Leo Jijinin Dar es salaam Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Atupele Mwakibete wakati wa hafla ya kupokea mabehewa 6 ya ghorofa kati ya 30 yaliyotokea nchini Ujerumani kwa ajili ya abiria ambapo yalifanyiwa maboresho na Kampuni ya Luetkemeyer Transport Logistic (GMBH) yaliyowasili jumanne ya wiki hii
“Mabehewa 6 ya gorofa mewasili ni sehemu ya mabehewa 30, ambayo yatahudumia abiria wa daraja la pili na la tatu, huku yakiwa na uwezo wa kubeba abiria 123 na 140. Mabehewa 24 yaliyosalia na vichwa viwili vitawasili nchini baada ya matengenezo kuwa yamekamilika” amesema Mwakibete
“Safari za treni ya umeme itaanza safari mwezi wa saba baada ya kichwa kimoja kufika na kichwa kingine kitafika na mabehewa mabehewa 24 yanayoendelea kutengenezwa hivyo wananchi wasiwe na hofu kuona treni hiyo imetumia muda mwingi kuanza sababu ni kutokana na seriksli ilivunja mkataba na kampuni ya kwanza” amesema Naibu Waziri
Kwa upande wake Msemaji wa serikali Gryson Msigwa amesema jambo hilo ni la kipekee limesubiriwa na wananchi kwa muda mrefu hivyo sasa leo Mabehewa 6 ya gorofa kati ya 30 yamepokelewa na ni ya daraja la pili la tatu Yana uwezo wa kubeba abiria 123 na daraja la tatu abiria 140 hivyo ni vitendea kazi vilivyokuwa vikisubiriwa ili majaribio yaanze kisha safari ya kusafirisha abiria kuanzia Dar es salaam mpaka Morogoro na itasafiri kilometa 160 kwa saa Moja.
“Wizara ya ujenzi uchukuzi kupitia Shirika la Reli TRC itasimamia Mkataba iliyosainiwa ya ununuzi wa vifaa ikiwemo mabehewa 59 kutoka Korea, mabehewa ya mzigo 1,430 kutoka China na vichwa vya treni EMU seti 10″ amesema Msemaji wa Serikali
Amesema nchini zaidi tano zimeonyesha utayari wa kujenga reli ya kisasa kiwango cha kimataifa (SGR) kupitia ubia katika ushoroba wa Mtwara ili kuchochea ukuaji wa uchumi nchini.
Nae Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Reli Tanzania (TRC), Masanja Kadogosa alimshukuru Rais Dk. Samia Suluhu kwa kusimamia shirika hilo na kutoa takribani Shilingi za kitanzania trilioni 23 kwa miradi ya ujenzi wa reli.
“Mabehewa hayo ni ya kisasa na yamegharimu euro milioni 26.6 huku behewa moja la gorofa ni sawa na abiria wa mabasi matatu na kitakachofuata sasa ni kichwa cha treni ambacho kinatarajia kufika Julai mwishoni kianze kufanya kazi mwaka huu,” amesema Kdogosa.








