Home Kitaifa BRELA YAWANOA WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI

BRELA YAWANOA WAHARIRI NA WAANDISHI WA HABARI

Na Magrethy Katengu

Mwenyekiti wa Jukwaa la Wahariri Tanzania TEFF Deodatus Balile amesema Vyombo vya habari ni nyenzo muhimu kusaidia wananchi kupata taarifa sahihi hivyo BRELA kwa kutambua hilo wameitisha semina kwa Wahariri na waandishi wa habari kwa kuwapatia elimu itakayosaidia kuhamasisha biashara nchini

Akizungumza leo jijini Dar es salaam katika warsha ya Uhamasishaji wa utekelezaji wa kanuni za wanufaika wa mwisho katika kampuni ambapo amesema Wakala wa Usajili wa bishara wa biashara na lesen (BRELA) ambapo amesema walio wengi hawana uelewa kuhusu mfumo unaotumika kusajili biashara na kampuni kwa njia ya mtandao wengine hawana uwelewa hivyo warsha hii ya leo itakuwa chachu kwa wahariri na waandishi kuandika na wananchi kupata elimu..

Sisi Tunashukuru kuona BRELA kwani imekuwa ikiwashirilisha wanahabari hususani wahariri kwenye shughuli zake mbalimbali zinazohusu utendaji kazi kila siku hii ni pamoja na marekebisho , maboresho yanayoendelea ya kisheria na kimfumo ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata taarifa sahii kuhusu mabadiliko hayo yenye lengo la kuboresha huduma zinazotewa na urahisi wa kuzitumia huduma hizo kufanya bishara nchini” amesema Balile

Kwa upande wake Mwakilishi Usajili BRELA Isdor Mkindi amesema kupitia warsha hii kuwaeleza wahariri wa vyombo vya habari utekelezaji wa umiliki na kuwaomba wasidie kupeleka ujumbe kwa Makampuni na wafanyabishara kuhuisha taarifa za kampuni na majina ya bishara mtandaoni inaendelea hivyo inaendelea kufanyika kwa njia ya mtandao.

Hata hivyo amesema kwa sasa muamko ni Mzuri wa usajili majina ya makampuni na biashara baada ya kuingia mtandaoni kwani hapo awali ilikuwa ni ngumu kutokana na kulazika kufika ofisini ndiyo mwananchi apate huduma ya usajili lakini sasa imerahisishwa mtu anaingia katika tovuti popote alipo na kujisajili kimtandao .

Dunia sasa ipo kidigitali zaidi hivyo kupitia kampeni yetu ya kuhuisha taarifa za makampuni itafanikiwa na ni rahisi sana na tangu 2018 tulipoanza kutumia kila kitu kwa mtandao lakini licha ya changamoto ya kusuasua lakini zoezi linaendelea vizuri hivyo kupitia warsha hii tunaamini Wahariri watatusaidia sana” amesema Mkindi

Naye Mhariri Mkuu gazeti la habari leo Mgaya Kingumba amesema Brela ilichokifanya ni cha pekee kwani Dunia iko Kidigitali na inawasaidia Wananchi kuwapunguzia muda wa kutembea kufuata ofisi zao na kuondoa utakatishaji wa taarifa hivyo wataitumia semina hiyo vizuri kuelimisha Wananchi

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!