Home Kitaifa RAIS DKT. MWINYI KUSHIRIKI JUKWAA LA KIMATAIFA LA TATU LA UCHUMI NCHINI...

RAIS DKT. MWINYI KUSHIRIKI JUKWAA LA KIMATAIFA LA TATU LA UCHUMI NCHINI QATAR

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi ameondoka Zanzibar leo tarehe 21 Mei 2023 kuelekea nchini Qatar kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan katika Jukwaa la Kimataifa la tatu la Uchumi linalofanyika jijini Doha.

Jukwaa hilo linalodhaminiwa na Kampuni ya Kimataifa ya Bloomberg lenye kauli mbiu isemayo “Simulizi za Ukuaji Kimataifa“ ambalo hufanyika nchini Qatar kila mwaka.

Mkutano huo unatarajiwa kuhudhuriwa na maelfu ya washiriki ikiwa ni pamoja na viongozi wa kampuni kubwa duniani, viongozi wa juu wa Serikali, na pia mamlaka zinazohusika za Qatar.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!