Na Magrethy Katengu
Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania (TanTRADE) imesema maonyesho ya mwaka huu yatakuwa ya kipekee sana kwani jumla ya nchi 14 zimethibitisha kushiriki katika maonyesho ya 47 ya Biashara ya kimataifa DITF maarufu sabasaba huku kampuni za ndani 1188 na kampuni za nje112 .
Akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar es salaam Kaimu Mkurugenzi Mamlaka ya Maendeleo ya biashara Tanzania TanTrade Fortunatus Mhambe amesema maonyesho hayo yatakuwa na yakifanyika katika viwanja vya Sabasaba 2023 kuanzia juni 28- Julay 13 Jijini Dar es salaam ambapo wafanyabiashara watapata fursa za kutangaza bidhaa zao wanazozalisha na kubadilishana uzoefu wa masoko ndani na nje ya nchi maonyesho hayo yataendeshwa na kauli mbiu ya “Tanzania ni mahali sahihi pa biashara na uwekezaji “ ikisisitiza Makampuni, Wafanyabiasha kujisajili kujisajili wasikose fusra.
“Hii ni nafasi nzuri kwa Makampuni na Wafanyabiashara wa ndani kukuza biashara zetu kujenga mtandao wa kibiashara na kuimarisha mchango wetu katika maendeleo ya nchi yetu,kwanin kushiriki katika maonesho haya itasaidia kuleta mabadiliko chanya katika sekta za kibiashara na uchumi kwa ujumla” ,amesema Mhambe..
Hata hivyo amezungumza kuhusu sabasaba ExpoVillage ambayo ni moja kati ya program za maonesho ya DITF ,eneo hili limejitolea kutangaza fursa zilizopo katika sekta ya madini,Tehama ,Gesi na mafuta ,siku ya mazingira, sanaa pamoja vijana na wanawake”Mhambe.
Amesema Expo Village tunaweza kuonyesha uwezo wetu wa ubunifu na uvumbuzi eneo hili linatoa fursa kwa wajasiriamali hasa vijana na wanawake kuonyesha talanta zao na kushiriki katika shughuli za biashara ,hii ni njia ya kukuza ujasiriamali na kuwapa fursa sawa wadau wote katika sekta ya biashara.









