Home Kitaifa Ewura Yatoa Elimu, Yapokea Mrejesho Kuhusu Matumizi Ya Gesi Asilia Iliyokandamizwa Dar...

Ewura Yatoa Elimu, Yapokea Mrejesho Kuhusu Matumizi Ya Gesi Asilia Iliyokandamizwa Dar Es Salaam

Celebrating 25 Years of NHIF

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) leo 25 Novemba 2026 imetoa elimu kwa madereva bajaji, magari yanayotumia gesi asilia iliyokandamizwa (CNG) na umma kwa ujumla kuhusu kanuni za usalama, katika eneo la kituo cha CNG cha TPDC, Sam Nujoma Dar es Salaam.

FAHARI AFYA

Madereva hao, pamoja na mambo mengine wamekumbushwa kuvifanyia ukaguzi vyombo vyao vya usafiri kwa kuzingatia utaratibu, kuhakikisha hakuna mivujo ya gesi na kutoweka mizigo juu ya mtungi wa CNG kwani inaweza kusababisha uharibifu.

Aidha, EWURA imetumia fursa hiyo kupokea mrejesho kuhusu huduma za CNG katika vituo ambapo madereva wameeleza kuwa, kwa ujumla hali ya utoaji huduma ni ya kuridhisha isipokuwa wapo baadhi ya wahudumu wenye kauli ziziso za staha,hivyo kuiomba EWURA kufuatilia na kuchukua hatua stahiki.

Vilevile, wameitaka EWURA kuendelea kuhamasisha uwekezaji katika vituo vya CNG ili kupanua wigo wa huduma hususan kuanzia Ubungo hadi Kibamba ambapo hakuna kituo kwa sasa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!