
Na Mwandishi Wetu-Mzawa BLOG
KLABU ya Al Ahly ya Misri imemfuta kazi kocha wake mkuu, Hussein Ammouta, kufuatia kipigo ilichopata jana dhidi ya Pyramids FC, hatua inayotajwa kuwa sehemu ya mabadiliko ya benchi la ufundi baada ya matokeo hayo.
Ammouta, ambaye aliteuliwa kuiongoza Al Ahly Juni 8 mwaka huu, amedumu kwa muda mfupi katika nafasi hiyo kabla ya uongozi wa klabu hiyo kuamua kusitisha huduma zake.
Uamuzi huo umefanyika baada ya timu hiyo kushindwa kupata matokeo iliyokuwa ikiyahitaji katika mchezo dhidi ya Pyramids, ambao umeongeza presha kwa benchi la ufundi.
Kuondoka kwa Ammouta kunafungua ukurasa mpya kwa Al Ahly katika kipindi ambacho klabu hiyo inahitaji kurejesha ushindani na kuimarisha mwenendo wake katika mashindano inayoshiriki.
Kwa Matokeo hayo ya mabao 2-0 ,Al Ahly anashuka mpaka nafasi ya tatu akiwa na Pointi 20 akiwa amecheza mechi tisa ,Nafasi ya pili Zamalek wakiwa na Pointi 22 wakicheza mechi tisa huku Pyramids FC ikiendelea kuongoza usukani wa Ligi wakiwa na Pointi 27 wakiwa wamecheza mechi tisa.









