Home Kitaifa GBT YAIKARIBISHA BETSASA SOKONI, YAITAKA KUZINGATIA MAADILI

GBT YAIKARIBISHA BETSASA SOKONI, YAITAKA KUZINGATIA MAADILI

Celebrating 25 Years of NHIF

Na Magrethy Katengu – Mzawa Media
Dar es Salaam

MKURUGENZI Mkuu wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha (GBT), James Mbalwe, ameikaribisha kampuni mpya ya BetSasa na kuitaka kuzingatia maadili na ustawi wa vijana kwa maendeleo ya jamii.

FAHARI AFYA

Mbalwe ameyasema hayo leo, Novemba 18, 2026, jijini Dar es Salaam, wakati wa uzinduzi wa kampuni ya BetSasa na kampeni ya kuwazawadia wateja wa kampuni hiyo zawadi mbalimbali, ikiwemo gari jipya aina ya Jetour.

“Tunawakaribisha BetSasa katika soko la Tanzania. Tumeona wameanza vizuri kwa kuja na kampeni hii inayolenga kuwazawadia wateja wao zawadi zenye thamani kubwa, ikiwemo gari jipya la kisasa.

“Hata hivyo, tunatoa wito kwao na kampuni nyingine katika sekta hii kuongeza tija ya shughuli zao kwa kuhakikisha wanarejesha kwa jamii kwa kusaidia sekta za afya, elimu, michezo na maeneo mengine muhimu ya maendeleo,” amesema Mbalwe.

Naye Ofisa Mtendaji Mkuu wa BetSasa, Jimmy Kenneth, amesema kampeni hiyo ya mwaka mmoja iitwayo ‘Kusanya Point Usepe na Jetour‘ inahusisha zawadi mbalimbali, zikiwemo fedha taslimu.

“Promosheni hii ni mahususi kwa wadau na wateja wa BetSasa, hivyo kila wiki zitatoka zawadi mbalimbali na kila baada ya miezi mitatu mshindi mmoja atapata gari jipya aina ya Jetour,” amesema Kenneth.

Kwa mujibu wa Ofisa Mtendaji Mkuu huyo, BetSasa imejipanga kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia sheria, kanuni, masharti, taratibu na miongozo ya mamlaka zinazosimamia michezo ya kubahatisha na kutekeleza wajibu wake kwa jamii.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!