Home Kimataifa TANZANIA YATAKA MIUNDOMBINU IWE KICHOCHEO CHA MTANGAMANO WA AFRIKA

TANZANIA YATAKA MIUNDOMBINU IWE KICHOCHEO CHA MTANGAMANO WA AFRIKA

Tanzania imetaka nchi za Afrika kuongeza kasi ya kuunganisha miundombinu ya usafiri, nishati na mifumo ya kidijitali ili kurahisisha biashara, kuimarisha minyororo ya thamani na kujenga uchumi wa bara wenye uwezo wa kukabiliana na misukosuko ya kimataifa.

Wito huo umetolewa na Makamu wa Rais, Mhe. Deogratius John Ndejembi, wakati akihutubia Mkutano wa 8 wa Kamati ya Uratibu ya Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Afrika, El Alamein, Misri, Oktoba 4, 2026.

Amesema Tanzania inaendelea kuimarisha miundombinu ya usafiri, ikiwemo TAZARA, SGR inayounganisha Tanzania na Burundi na DRC, pamoja na kuboresha bandari na huduma za usafiri wa anga.

Aidha, Tanzania inaendelea na miradi ya kusafirisha umeme inayolenga kuunganisha EAPP na SAPP, pamoja na miradi ya pamoja ya uzalishaji umeme na Burundi, Rwanda na Uganda.

Ndejembi ametangaza nia ya Tanzania kupendekeza Kaulimbiu ya Mwaka 2028 ya Umoja wa Afrika: “Kuunganisha Mataifa: Kuharakisha Mtangamano wa Kiuchumi wa Afrika kupitia Miundombinu.”

Amesema pendekezo hilo linalenga kuongeza msukumo wa kisiasa katika kuunganisha miundombinu, kuboresha biashara mipakani, kupunguza gharama za usafirishaji na kuunga mkono utekelezaji wa Agenda 2063 na AfCFTA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!