Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Viwanda, Biashara, Kilimo na Mifugo ikiongozwa na Mwenyekiti, Mhe. Deodatus Mwanyika (Mb), imeridhia Randama ya mpango wa bajeti ya makadirio ya mapato na matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa fedha 2026/2027 Machi 26, 2027 Bungeni jijini Dodoma
Katika michango yao, Wajumbe wa Kamati hiyo walionyesha kuridhishwa na vipaumbele vya Mpango wa Bajeti hiyo ya mwaka 2026/2027, huku wakimpongeza Waziri Kapinga kwa uwasilishaji wenye maono mapana yanayolenga kukuza sekta ya viwanda na biashara nchini. Pamoja na pongezi hizo, Kamati ilitoa miongozo na ushauri wa kimkakati uliolenga kuboresha mazingira ya biashara, na viwanda nchini.
Naye, Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Judith Kapinga (Mb), alibainisha kwa kina kuwa vipaumbele vya kimkakati vitakavyopewa uzito katika Mpango wa bajeti wa 2026/2027, pamoja na mchanganuo wa fedha zinazohitajika kutekeleza majukumu hayo.
Uidhinishaji wa makadirio hayo unafungua milango kwa Wizara ya Viwanda na Biashara kuanza maandalizi ya mwisho ya Hotuba ya Bajeti itakayowasilishwa rasmi na katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa Mkutano wa bajeti.























