Home Kitaifa MGOMBEA UBUNGE NLD AIKUMBUSHA SERIKALI KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI

MGOMBEA UBUNGE NLD AIKUMBUSHA SERIKALI KUWAINUA VIJANA KIUCHUMI

Na Boniface Gideon, Tanga

Aliyekuwa mgombea ubunge wa Jimbo la Tanga katika uchaguzi mkuu uliofanyika Oktoba 29, 2025 kupitia chama cha National League for Democracy (NLD), Ramadhani Mwikalo, ameitaka serikali kuwakumbuka vijana kwa kuwawezesha kiuchumi hususani katika sekta ya teknolojia ili kupunguza tatizo la ukosefu wa ajira.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Tanga, mara baada ya kuwasili nchini akitokea China alikohudhuria Mkutano Mkuu wa Mwaka wa kampuni ya Sinoma (Suzhou) Construction Co., Limited inayojihusisha na ujenzi wa miundombinu mbalimbali ya viwanda, vituo vya gesi, na usafirishaji.

Mwikalo alisema, endapo taifa litaweka mikakati imara ya kuwawezesha vijana nchini hususani katika sekta ya teknolojia ni rahisi zaidi kuondoa changamoto za ukosefu wa ajira nchini.

Sote tunaona kwenye mataifa ya wenzetu wamewekeza sana kwenye teknolojia, hii imewasaidia sana kwenye mataifa yao kuongeza kiwango cha ajira, vijana wamekuwa wabunifu wa kutengeneza bidhaa mbalimbali kuanzia wakiwa wadogo, hii imewasaidia kuinua uchumi wa nchi zao na uchumi wa vijana wenyewe,” aliongeza Mwikalo.

Alisema mkutano huo wa wiki moja uliwakutanisha viongozi, wataalamu na wadau mbalimbali. Miongoni mwa ajenda kuu zilizojadiliwa ni fursa za uwekezaji katika sekta za ujenzi na uchimbaji madini, sekta ambazo zimeendelea kuwa mhimili muhimu wa maendeleo ya taifa.

Tumejadiliana kwa undani fursa za uwekezaji katika ujenzi na madini na namna teknolojia inavyochukua nafasi kubwa katika sekta ya uchumi duniani, hivyo nitumie fursa hii kuikumbusha serikali, kuona umuhimu wa kuwawezesha vijana nchini katika teknolojia ili kuimarisha uchumi wao,” alisisitiza Mwikalo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!