
Kampeni ya Kitaifa ya uwezeshaji uwekezaji wa ndani ni utekelezaji wa Vitendo wa Dira ya Taifa ya 2050 na Ilani ya CCM 2025-2030 ambayo inalenga kutekeleza adhma ya dhati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuhamasisha uwekezaji wa ndani na nje ya nchi katika fursa zilizopo kwenye sekta mbalimbali.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe.Judith Kapinga wakati wa Ufunguzi wa Kongamani la Uwekezaji Kanda ya Ziwa, Februari 04,2026 Jijini Mwanza, ambapo
amebainisha kuwa Tanzania imeendelea kuimarisha imani kwa Wawekezaji wa ndani na wa Kimataifa kwa kuweza kuondoa vikwazo vya kiutawala na kuweka mazingira wezeshi yanayochochoe ustawi na ukuaji ya uchumi na maendeleo ya biashara kupitia sekta ya biashara na uwekezaji.

Kapinga amesema lengo la serikali ni kuhakikisha Tanzania inakuwa miongoni mwa nchi tatu bora barani Afrika katika kuvutia uwekezaji na kuwa na mazingira bora ya kufanya biashara ifikapo mwaka 2050.
Waziri Kapinga amebainisha kuwa Lengo la kampeni hiyo ni kubadili fikra za na Watanzania ya kuamini mwekezaji ni mgeni tu na si watanzania hivyo kutoa elimu ya uwekezaji kwa makundi mbalimbali na kuongeza hamasa itakayosaidia kuleta muamko na kuongeza idadi ya wawekezaji wa ndani kuanzia Halmashauri, Wilaya na Mikoa yote.
Waziri Kapinga amesema kama Wizara ya Viwanda na Biashara kupitia Tassisi za BRELA,TBS, WMA, SIDO, TANTRADE na FCC imeendelea kuboresha na kuimarisha mazingirabya uwekezaji kwa kurahisisha mifumo ya usajili hususani kwa kanda ya ziwa mradi wa maabara za tbs umeanza ili kurahisisha upatikanaji wa huduma kwa kandanhiyo.

Aidha ameielekeza TISEZA kuendelea na kampeni hiyo ili Watanzania waweze kuelewa dhana nzima ya uwekezaji wa ndani na kushirikiana kikamilifu na Sekretarieti za Mikoa na Sekta binafsi zote binafsi ili kufikia dhamira ya dhati ya Serikali.
Nae Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mtanda amesema kuwa kwa sasa Mkoa huo unapokea Wafanyabiashara wengj kutoka nje ya nchi kutoka Kenya, Uganda, Congo, Burundi na Rwanda na imani kubwa ni kuwa watafanyabiashara hao wataongezeka.








