Home Kitaifa BILIONI 45.8 KUTUMIKA KUFIKISHA UMEME KATIKA VITONGOJI MKOANI SIMIYU

BILIONI 45.8 KUTUMIKA KUFIKISHA UMEME KATIKA VITONGOJI MKOANI SIMIYU

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo,akizungumza wakati wa kikao cha kumtambulisha rasmi Mkandarasi wa Mradi huo Burhani Engineers limited atakaye hudumia Vitongoji 415 vya Mkoani wa Simiyu kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anamringi Macha.

Na.Mwandishi Wetu-SIMIYU

Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu Bi. Prisca Kayombo akimwakilisha Mkuu wa Mkoa huo Mhe. Anamringi Macha ametoa rai kwa Wanachi Mkoani Simiyu kuchangamkia fursa ya umeme Vitongojini wenye thamani ya kiasi cha Shil Bil. 4.8 unaotekelezwa na Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Bi. Kayombo pia amewataka wananchi kutokuhujumu miradi hio kwani lengo lake ni kukuza na kuinua uchumi wa mwananchi mmoja mmoja na Mkoa kwa ujumla.

Ameyasema hayo leo tarehe 04/02/2026 Ofisini kwake wakati wa kikao cha kumtambulisha rasmi Mkandarasi wa Mradi huo Burhani Engineers limited atakaye hudumia Vitongoji 415 vya Mkoani wa Simiyu.

Aidha, Bi. Kayombo amewasisitiza wananchi wa Mkoa huo kutoa ushirikiano kwasababu mradi huo unakwenda kupelekea Maendeleo ya kiuchumi katika Mkoa huo.

“Mradi huu utakwenda kusaidia uendeshaji wa viwanda vidogo, Umeme utakwenda kurahisisha uchimbaji wa Dhahabu na kusaidia katika viwanda vya uchakataji wa zao la Pamba na mafuta ya kupikia ya Alizeti.

“Hii Miradi ni Miradi ya Maendeleo hivyo Wananchi mtoe ushirikiano kwa asilimia kubwa. Lakini sisi pia ni wakulima wazuri wa zao la alizeti na pamba, nahakika umeme huu utasaidia katika viwanda vitakavyo tengeneza mafuta yakupikia yatokanayo na alizeti” amesisitiza Bi. Kayombo.

Kwa upande wake, Mhandisi Seif Abduli, Mhandisi wa Miradi kutoka Wakala wa Nishati Vijijini (REA) amesema kwa Mkoa wa Simiyu Jumla ya Vitongoji 415 vitaanza kufikishiwa Umeme huku taratibu zingine zikiendelea ili kabla ya 2030 Vitongoji Vilivyo bakia 1026 vinafikiwa na Umeme

Mhandisi Seif ameeleza kuwa Vitongoji hivyo Vitahusisha kuunga Wateja 13292 na Mradi utatekelezwa kwa Muda wa Miaka Mitatu hivyo ametoa wito kwa Wananchi kuhakikisha kwamba wanachangamkia Fursa ya kuanzisha viwanda vidogo vidogo vitongojini kwani transformer zitakazo fungwa zitakuwa na uwezo wa kukidhi mahitaji ya viwanda.

Mhandisi Seif amesema kuwa Serikali inatumia gharama kubwa ya kufikisha huduma ya umeme kwa wananchi wake, hivyo akawataka kila mwananchi awe mlinzi wa miundombinu hiyo ili malengo ya kuwainua wananchi vijijini kiuchumi na kijamii yaweze fikiwa.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!