Home Kitaifa MAKONDA AWATAKA MAOFISA HABARI KUSAMBAZA HABARI SAHIHI ZA SERIKALI

MAKONDA AWATAKA MAOFISA HABARI KUSAMBAZA HABARI SAHIHI ZA SERIKALI

Na Secilia Edwin

DODOMA – Maofisa habari wa serikali wametakiwa kuhakikisha wanazifikisha kwa wananchi habari na taarifa sahihi za utekelezaji wa shughuli za serikali ili kuondoa upotoshaji na kuwajengea wananchi uelewa wa mambo yanayofanyika nchini.

Hayo yamesemwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, Desemba 15, 2025 jijini Dodoma, alipokuwa akizungumza na Menejimenti ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo katika Ofisi za Wizara, Mji wa Serikali Mtumba, jijini Dodoma, ambapo alisisitiza kuwa maofisa habari wana wajibu wa kuwa mstari wa mbele katika kutoa ufafanuzi wa masuala ya serikali kwa wakati na kwa usahihi.

Alisema hatua hiyo ni muhimu kwani taarifa potofu zimekuwa zikisambaa kwa kasi, hususan kupitia mitandao ya kijamii, hali inayoweza kupotosha jamii na kupunguza imani ya wananchi kwa serikali iwapo hakutakuwa na maelezo sahihi kutoka vyanzo rasmi.

Aidha, aliwahimiza maofisa habari kutumia vyombo mbalimbali vya mawasiliano, ikiwemo redio, televisheni, magazeti na mitandao ya kijamii, ili kufikisha ujumbe wa serikali kwa wananchi, huku akisisitiza weledi, uwazi na uzingatiaji wa maadili ya taaluma ya habari.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!