



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Balozi Dkt. Emmanuel Nchimbi, amewasili Jijini Lusaka, Zambia, leo Novemba 19, 2025, kwa ajili ya kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi kuashiria uzinduzi wa ukarabati mkubwa wa Reli ya TAZARA unaotarajiwa kufanyika tarehe 20 Novemba 2025.
Akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kenneth Kaunda, Makamu wa Rais alipokelewa kwa heshima na Waziri wa Afya wa Jamhuri ya Zambia, Mhe. Dkt. Elijah Muchima, pamoja na Balozi wa Tanzania nchini Zambia, Mhe. Balozi Luteni Jenerali Mathew Mkingule. Kadhalika, maafisa waandamizi wa Serikali ya Zambia na Tanzania walihudhuria mapokezi hayo, yakipambwa na vikundi vya ngoma vilivyoandaliwa mahsusi kwa ajili ya kumkaribisha.
Katika ziara hiyo, Makamu wa Rais Mhe. Dkt. Nchimbi ameambatana na viongozi kadhaa akiwemo Katibu Mkuu wa Wizara ya Uchukuzi, Prof. Godius Kahyarara, Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Reli Tanzania (TRC), Mhandisi Machibya Masanja, pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa TASAC, Bw. Mohamed Salum









