Home Kitaifa DKT. MWINYI AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA ZANZIBAR SPORTS CITY

DKT. MWINYI AKAGUA MAENDELEO YA MRADI WA ZANZIBAR SPORTS CITY

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ametembelea mradi wa kimkakati wa Zanzibar Sports City kukagua maendeleo ya ujenzi unaoendelea kwa maandalizi ya AFCON 2027.

Serikali imeihakikishia Wizara ya Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo pamoja na Kampuni ya ORKUN GROUP kuwa itaendelea kuweka mazingira wezeshi kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa kasi, ufanisi na viwango vya Kimataifa.

Katika ziara hiyo, Rais Dkt. Mwinyi aliambatana na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Mhe. Riziki Pemba Juma, pamoja na Naibu Waziri, Mhe. Ali Abdulgullam Hussein.

Ujenzi wa Zanzibar Sports City ni sehemu ya mkakati wa Serikali wa kuimarisha miundombinu ya michezo na kuongeza uwezo wa Zanzibar kuandaa mashindano makubwa ya Kimataifa.

Awamu ya kwanza inahusisha:
● Uwanja wa Kimataifa wa Mpira wa Miguu wenye uwezo wa mashabiki 36,500
● Viwanja viwili vya mazoezi vyenye uwezo wa mashabiki 15,000
● Uwanja maalum kwa sherehe za Kitaifa

Mradi unatarajiwa kukamilika Disemba 2026.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!