Na Magreth Mbinga
Utalii ni biashara ambayo inatufanya tuwe wamoja sababu tunavivutio vya kutosha wote tukiwa mabalozi kutangaza Utalii tutafika mbali.
Hayo yamezungumzwa na Waziri wa Utalii na Mambo ya Kale Zanzibar Mhe. Simai Mohammed Said katika hafla ya uzinduzi wa CROWN PLAZA AN IHG HOTEL ya Jijini Dar es Salaam na kusema kuwa anaamini itajengwa tena Bagamoyo na Tanga ili kuungana na Saadani pamoja na Zanzibar.
“Historia iliyokuwepo wakati wa Ukoloni na kuisha haiwezi kubadilika tuzithamini nyumba za kihistoria za Dar es Salaam ili kufanya kuwa mji wa kihistoria” amesema Mhe. Simai.
Pia Mhe. Simai amesema kujengwa kwa hotel hiyo kutafungua fursa nyingi sana kwa Wakazi wa Dar es Salaam kila mwenye rasilimali yake aitunze sana .
“Hotel hii ni nzuri sana pia ni kiunganishi cha maeneo mengi katika Jiji hili sababu ipo katikati ya mji inakuwa rahisi kufika eneo lolote kwa urahisi” amesema Mhe. Simai.
Aidha Mh Simai amewataka Watanzania kufanya Utalii wa bahari hasa wakati huu wa joto waende wakaangalie nyangumi sambamba na kufanya matembezi ya bahari ili kujionea rasilimali zilizopo baharini.