Home Kitaifa MHE. NGOMA: TUACHE USIRI, TUFUNGUKE ELIMU YA UKIMWI

MHE. NGOMA: TUACHE USIRI, TUFUNGUKE ELIMU YA UKIMWI

NA.MWANDISHI WETU

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma ameiasa jamii kubadili mitazamo juu ya utoaji wa elimu kuhusu masuala ya UKIMWI kwa vijana nchini ili kusaidia katika mapambano ya kudhibiti maambukizi ya Virisi vya UKIMWI.

Mkuu wa Wilaya ya Ruangwa Mhe. Hassan Ngoma akizungumza na vijana wakati wa mkutano wao katika kuelekea kilele cha Maadhimisho ya Siku ya UKIMWI Duniani yatakayofanyika tarehe 1 Desemba 2022 Mkoani Lindi

Ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na Vijana walishiriki katika Mkutano wa mwaka wa vijana, viongozi wa dini na wadau wanaotekeleza miradi ya vijana balehe na wanawake vijana uliofanyika katika ukumbi wa Sea View Beach Resort mkoani Lindi tarehe 26 Novemba, 2022.

Mkuu wa Wilaya alisema wazazi na walezi hawanabidi kubadili mitazamo iliyopo juu ya vijana wao na kuamini ni wadogo hawafai kupewa elimi ya masuala ya UKIMWI bila kujua mazingira yanayowazunguka ni hatarishi.

“Tunakosea sana kuona vijana hawa ni watoto hii si sahihi, ukweli ni kwamba ni wakubwa kimatendo na mwamko wao kuhusu umuhimu wa kulinda afya zao ni mdogo sana,” Mhe. Hassan

Aliongezea kuwa kukosekana kwa uwazi katika malezi umechangia kuharibu tabia za watoto kwani wameendelea kujiingiza katika matendo maovu bila wazazi kujali.

Aidha alieleza miongoni mwa sababu zinazochangia ongezeko la maambukizi mapya ya Virusi Vya UKIMWI kwa vijana ni Matumizi yasiyosahihi ya simu za mikononi yanachangia ongezeko la vishawishi vya kingono kwa vijana hivyo kupelekea kuzima ndoto zao.

Aliongezea kuwa kukosekana kwa taarifa za tahadhari katika familia zetu kumewafanya vijana kutokuwa na hofu juu ya uwepo wa ugonjwa huu.

“Hali ya maambukizi imeongezeka kwetu sababu watu wamekosa hofu kuhusu madhara ya uwepo wa virusi vya UKIMWI wakijitia moyo kwa uwepo wa kinga na matumizi ya dawa za kuzuia mimba,” alisisitiza Mhe. Hassan

Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa mwaka wa vijana, viongozi wa dini na wadau wanaotekeleza miradi ya vijana balehe katika ukumbi wa Sea View Beach Resort mkoani Lindi tarehe 26 Novemba, 2022 wakifuatilia mkutano huo.

Alitoa rai kwa vijana kuchukua mikakati madhubuti ikiwemo ya kubadili mitazamo na tabia.

“Namna pekee ya kutoka hapa ni kubadili tabia, na hii ni kazi ya familia zetu na viongozi wa kidini.Viongozi wa dini waendeleee kueleimisha tuone namna ya kuvunja ukimya,”alisistiza

Pia aliongezea kuwa kuwepo na mikakati sahihi inayoendana na mabadiliko ya kiteknolojia katika mapambana haya.

“Malengo hayatatimia kama mikakati ni dhaifu, hatuwezi kuwa na njia zile zile za mapambano bila kuwa na strategies mpya zinazoendana na mabadiliko haya ya kiteknolojia,”


=MWISHO=

Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti UKIMWI nchini Dkt. Leonard Maboko akizungumza wakati wa kongamano hilo
.
Baadhi ya washiriki wa Mkutano wa mwaka wa vijana, viongozi wa dini na wadau wanaotekeleza miradi ya vijana balehe wakiwasilicha hoja zao wakati wa mkutao huo

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!