Home Kitaifa WANANCHI MUSOMA VIJIJINI WAPOKEA ZAWADI YA SIKUKUU KUTOKA KWA RAIS DKT.SAMIA

WANANCHI MUSOMA VIJIJINI WAPOKEA ZAWADI YA SIKUKUU KUTOKA KWA RAIS DKT.SAMIA

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI wa jimbo LA Musoma vijini wamepokea zawadi ya sikukuu ya Krismass na mwaka mpya kutoka kwa Raid Dkt.Samia Suluhu Hassan.

Zawadi iliyotolewa ni gari la kubeba wagonjwa( Ambulance) lililokabidhiwa na mbunge wa jimbo hilo Profesa Sospeter Muhongo.

Gari hilo limekabidhiwa jana disemba 24 kwenye kituo cha afya cha Kata ya Bugwema na kupokelewa kwa shangwe na wananchi walioshuhudia tukio hilo.

Wanavijiji kutoka Kata hiyo yenye vijiji vinne vya (Bugwema, Kinyang’erere, Masinono na Muhoji) wamemshukuru sana Rais Dkt.Samia kwa kuwapatia gari jipya la wagonjwa ambalo litawasaidia kwa huduma za afya.

Wanavijiji hao wameahidi kumpatia Rais Samia kura zote za Kata hiyo kwenye uchaguzi mkuu wa mwakani (2025).

” Tunamshukuru sana Rais Dkt.Samia kwa zawadi hii nzuri kwetu na tuna muombea maisha marefu ili aendelee kutuhudumia watanzania”anasema Musa Jumapili.

Akikabidhi gari hilo mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo amesema Rais Samia anawapenda na kuwathamini wananchi wa jimbo hilo na kutoa zawadi za mara kwa mara.

Amesema malipo pekee ni kumpa kura zote za jimbo hilo kwenye uchaguzi wa mwaka 2025 muda ukifika.

Hili linakuwa gari la 7 linalotoa huduma za afya jimbo la Musoma vijijini ambapo mbunge Muhongo amekuwa akisjirikiana pia na wadau mbalimbali kufanikisha kupatikana kwa magari hayo.

Aidha wanavijiji wanaendelea na ujenzi wa zahanati mpya 17 baadhi ya hizi zahanati tayari zimeanza kupokea michango ya fedha kutoka serikalini huku wito ukitolewa kwa wadau kuendelea kuchangia.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!