Home Kitaifa WANANCHI MKOANI SIMIYU WAPATIWA ELIMU YA UMEME NA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

WANANCHI MKOANI SIMIYU WAPATIWA ELIMU YA UMEME NA NISHATI SAFI YA KUPIKIA

Wakala wa Nishati Vijijini (REA) umeongeza kasi katika utoaji wa elimu kwa wananchi kuhusu matumizi salama ya umeme na umuhimu wa matumizi ya nishati safi ya kupikia katika Mkoa wa Simiyu.

Utoaji wa elimu hiyo unalenga kuwawezesha wananchi kuelewa fursa zinazotokana na upatikanaji wa umeme, matumizi sahihi na salama ya nishati hiyo, pamoja na kuwahamasisha kutumia nishati safi ya kupikia kama vile gesi, umeme na majiko banifu.

Kupitia kampeni hiyo ya uelimishaji, wananchi wanaendelea kupata ufafanuzi kuhusu namna ya kutumia umeme kwa usalama, kuepuka kuunganisha umeme kwa njia zisizo salama na umuhimu wa kutumia wataalamu wenye sifa katika kazi za ufungaji na matengenezo ya mifumo ya umeme.

Aidha, REA inaendelea kuhamasisha wananchi kuhusu faida za nishati safi ya kupikia katika kulinda afya za familia na mazingira, huku ikisisitiza umuhimu wa jamii kuchangamkia fursa za matumizi ya nishati hiyo katika shughuli za kila siku.

Elimu hiyo pia inawapa wananchi fursa ya kupata majibu ya maswali mbalimbali kuhusu huduma za umeme na nishati safi ya kupikia, hatua inayosaidia kuongeza uelewa na matumizi sahihi ya huduma hizo.

REA inaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali katika kuhakikisha elimu ya nishati inawafikia wananchi katika maeneo mbalimbali ya Mkoa wa Simiyu, ikiwa ni sehemu ya juhudi za Serikali za kuongeza matumizi ya nishati safi na kuboresha maisha ya wananchi.

Hatua hiyo inaendana na Mkakati wa Taifa wa Nishati Safi ya Kupikia, unaolenga kuhakikisha asilimia 80 ya Watanzania wanatumia nishati safi ya kupikia ifikapo mwaka 2034.

Mwisho

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!