Home Kitaifa WAFUGAJI TARAFA YA NANYUMBU WASISITIZWA KUJITOKEZA KUHESABIWA NA KUACHANA NA DHANA POTOFU...

WAFUGAJI TARAFA YA NANYUMBU WASISITIZWA KUJITOKEZA KUHESABIWA NA KUACHANA NA DHANA POTOFU JUU YA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2022

Tar.26.07.2022.

Ikiwa zimesalia siku chache sensa ya Watu na Makazi kufanyika Leo Afisa Tarafa Nanyumbu ndg. Livinus Nchimbi amefanikiwa kuwafikia Wafugaji wote ndani ya Tarafa na kuwapa Elimu ya umuhimu wa Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2022.

Ndg. Nchimbi amesisitiza kuwa kuna umuhimu mkubwa sana ya wao kama Wananchi kufahamika na kuhewasibiwa ili Serikali iweze kutekeleza vilivyo Shughuli mbalimbali za Maendeleo katika Jamii hiyo.

Huduma za Kijamii kama Elimu, Afya na hata za kiuchumi zinazohitajika kwa Wananchi,Serikali ni Lazima ijue takwimu sahihi ili kurahisha na kuwezesha upatikanaji wake kwa Wananchi.

Hivyo Siku hiyo ya tar.23. 08. Wakumbuke kuonesha Ushirikiano kwa kutoa taarifa zilizo sahihi kwa Maafisa watakaowafikia katika maeneo yao, kwani zoezi hilo halina uhusiano wowote na imani zinazodhaniwa na kufikiriwa kuwa wakihewabiwa watauzwa au watakufa. Hizo ni imani potofu na Afisa Tarafa aliwataka kuzipuuza Imani na Taarifa hizo

Kwa kulitambua hilo mjumbe mmoja aliyefahamika kwa jina maarufu la Bonge aliwaomba wafugaji wenzake kufikisha taarifa hizo katika kaya zao ili kusitokee hata kaya moja itakayokataa kutoa taarifa au kutoa taarifa zisizo sahihi.

Sambamba na hilo Afisa aliwataka WAFUGAJI hao kutokuwa sababu ya Kuchochea Migogoro kati yao na Wakulima kwa kupitisha au kuchunga Mifugo katika Mashamba ya Wakulima. Wanapaswa kuheshimu Taratibu na Sheria zilizopo ili kuendelea kuishi kwa Amani na kufanya shughuli za Maendeleo.

Mwisho walishukuru sana kwa ujio wa Afisa huyo na kuahidi Ushirikiano mkubwa katika siku hiyo ya Sensa Ambayo ni zoezi la Kitaifa.

#Tupeane maarifa kujenga Tz yetu#

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!