Na Shomari Binda-Musoma
WADAU na mashirika yasiyo ya kiserikali yametakiwa kutenga fedha kwenye bajeti zao kwaajili ya makuzi na malezi ya mtoto.
Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Mara Said Muhamed Mtanda kwenye uzinduzi wa Program Jumuishi ya Taifa ya Malezi,Makuzi na Maendeleo ya Mtoto (MMMAM).
Katika hotuba yake iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu wa wilaya ya Musoma,Dk.Khalfan Haule,amesema ili kumtunza mtoto yapo mambo ya kibajeti ambayo yanapaswa kutekelezwa.
Amesema ili kutekeleza mpango huo uliozinduliwa no vyema kila mmoja akaenda kutekeleza majukumu yake.
Mkuu huyo wa mkoa amesema malezi makuzi na maendeleo ya awali ya mtoto hayataweza kufanikiwa kama kutakuwa na vikwazo vya utekelezaji.
Amesema serikali ipo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali yakiwemo mashirika yasiyo ya kiserikali katika kufikia malengo ya mpango.
Aidha mkuu huyo wa mkoa amesema elimu watakayopata wadau waende wakaifanyie kazi katika kumsimamia mtoto.
Mratibu wa usimamizi wa mpango huo kutoka Kanisa la AIC Charles Mashauri amesema wamekuwa wakifanikiwa kwenye usimamizi wa program mbalimbali na kudai hilo pia litakwenda kufanikiwa.
Kwa upande wake mmoja wa washiriki wa uzinduzi huo mjumbe wa baraza la taifa la mashirika yasiyo ya kiserikali “NACONGO” Robby Samwel amesema malezi na makuzi ya kila mmoja ni jukumu la kila mmoja








