
Na Deborah Lemmubi-Dodoma.
MNEC wa kundi la Umoja wa Vijana Tanzania (UVCCM) na Mbunge wa Malindi Mhe Muhsin Ussi amesema kuwa Umoja huo utazidi kuongeza nguvu katika utoaji wa elimu ili kuwafikia vijana wengi zaidi bila kujali Itikadi zao cha Vyama kutokana na Mikakati iliyowekwa na Serikali kwani CCM kama Chama Tawala ina wajibu wa kuwaunganisha vijana wote.
Mhe Muhsin ameyasema hayo leo Jijini Dodoma November 15,2025 wakati akizungumza na Waandishi wa Habari kumpongeza Rais Dkt Samia Suluhu Hassan kwa Hotuba yake aliyoitoa November 14,2025 wakati akifungua Bunge la 13 kuwa imebeba upole,upendo na ukarimu kwa vijana na Watanzania kwa ujumla.

“Sisi kama umoja wa vijana tutaendelea na tutazidi kuongeza nguvu katika kutoa elimu ili kuwafikia viajana wengi zaidi,kuwagusa wote bila kujali itikadi zao za Vyama vya kisiasa,kwani chama cha Mapinduzi ikiwa ni Chama tawala kina wajibu wa kuunganisha wote wa nchi nzima.
Aidha ametumia nafasi hii kuwaomba kwa heshima na unyenyekevu baadhi wa wana Siasa ambao wameonesha kukataa mkono wa maridhiano alioutoa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dkt Samia Suluhu Hassan kuwa wawe na nia ya Kizalendo kwani Rais ameamua kusimama kama Mama ili kuliponya Taifa.
Hayo yamekuja mara baada ya Hotuba ya Rais aliyoitoa November 14,2024 akisema kuwa Serikali imetenga Shilingi Bilioni 200 kwaajili ya mipango ya vijana pamoja na mpango wa kuanzisha Wizara Maalum ya Vijana.








