Home Kitaifa UJENZI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI WAENDELEA KWA KASI JIMBO LA...

UJENZI WA MAABARA ZA MASOMO YA SAYANSI WAENDELEA KWA KASI JIMBO LA MUSOMA VIJIJINI

Na Shomari Binda-Musoma

WANANCHI wa jimbo la Musoma Vijijini wanaendelea kushirikiana na serikali kujenga maabara za masomo ya sayansi kwenye sekondari zao za kata.

Lengo la ujenzi wa maabara ni kuweza kupata wana sayansi ambao kwa sasa ni uhitaji katika soko la dunia.

Licha ya kupata wana sayansi ni kuongeza na kuboresha ufundishaji, uelewa na ufaulu mzuri kwenye mitihani ya masomo ya sayansi.

Katika taarifa iliyotolewa na ofisi ya mbunge wa jimbo la Musoma vijijini Profesa Sospeter Muhongo leo novemba 19 imesema sekondari zote zilizopo kwenye Kata 21 zinaendelea na ujenzi.

Taarifa hiyo imeeleza lengo pia ni kuongeza idadi ya High School ambapo kwa sasa ipo Kasoma High School yenye masomo ya “arts”na
Suguti High School yenye masomo ya sayansi kuanzia mwakani 2025 huku Mugango High School yenye masomo ya sayansi nayo kuanza mwakani 2025

(iv) Mtiro Sekondari (v) Makojo Sekondari
(vi) Kiriba Sekondari (vii) Etaro Sekondari

Aidha taarifa imedai kuwa ujenzi wa miundombinu ya elimu ya kuanzishwa kwa Mtiro High School unaendelea vizuri

“Michango ya thamani ya shilingi milioni 31 wachangiaji wakiwa wanakijiji, mbunge wa jimbo, mfuko wa jimbo na Halmashauri wamechangia”

“Mbunge wa jimbo la Musoma Vijijini, Prof Sospeter Muhongo, alipiga Harambee mbili (2) za kuanza ujenzi wa maabara hizo.

“Vyumba vipya 4 vya madarasa
Mchango wa shilingi milioni 100 mchangiaji serikali kuu na vyoo vipya
mchango shilingi milioni 24.9 mchangiaji akiwa pia serikali kuu” imesema sehemu ya taarifa hiyo.

Wananchi wa jimbo la Musoma Vijijini na viongozi wao wote wanaishukuru sana Serikali chini ya uongozi mzuri wa Mhe Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kuendelea kuchangia ujenzi wa miundombinu ya elimu kwenye sekondari zao za Kata na kuongeza idadi ya “high schools”, hasa za masomo ya sayansi.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!