Na Boniface Gideon,TANGA
Bodi ya Wakurugenzi Shirika la Petroli nchini ‘TPDC’,imeonyesha kuridhishwa na kasi ya ujenzi na matengenezo ya mradi wa Bomba la mafuta ghafi Afrika Mashariki ‘EACOP’,ambapo mradi huo umefikia asilimia 72 huku ukitarajiwa kuanza rasmi kufanya kazi ifikapo mwezi juni 2026.

Akizungumza na Waandishi wa Habari jana jijini Tanga mara baada ya Bodi hiyo kumaliza ukaguzi katika Wilaya zinazopitiwa na mradi huo katika Mkoa wa Tanga,
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya ‘TPDC’,Balozi Ombeni Sefue ,alisema mradi huo umeonyesha ukomavu wa mataifa mawili ya Afrika Mashariki katika sekta ya Uwekezaji,
”Mradi huu wa EACOP ,ndio mradi bora zaidi wa mafuta kwasasa Duniani,na umefuata taratibu zote za Kimataifa,mradi huu umeonyesha ukomavu na uimara wa mataifa ya Afrika mashariki“Alisisitiza Balozi Sefue

Balozi Sefue alisema,haikuwa kazi rahisi kupata mradi huo ,kutokana na Ushindani mkubwa uliokuwepo kwenye mataifa mbalimbali,
”Haikuwa rahisi kama nchi kuupata huu mradi kwa sababu chaguzi za njia ya kupitisha bomba zilikua nyingi na hivyo mafanikio ya kwanza kama nchi ni kufanikiwa kuupata huu mradi lakini kwa sasa kama nchi tumeendelea kunufaika zaidi kama vile kuongeza pato la Taifa pamoja na fidia nzuri walizolipwa watanzania waliopitiwa na mradi na kandarasi mbalimbali kwa makampuni ya kizalendo,” Alieza Balozi Sefue
Kwaupande wake ,mwakilishi wa mkurugenzi mkuu wa kampuni ya mafuta ghafi EACOP ,Georfrey Mponda ,alisema mradi huo ulianza rasmi utekerezwaji februali 15 mwaka 2022 na unatarajiwa kukamilika jun 2026 nakwamba mpaka sasa mradi huo umefikia 72% ya ujenzi ,
”Mradi huu umefikia 72% ya ujenzi wake,tunatarajia uanze kazi mwezi jun mwaka 2026,tunawashujuru sana wanahisa wote wakiwemo TPDC ,kwa ushirikiano wao,ni matarajio yetu kuwa mradi huu utaanza kazi kwa wakati” Alisema Mponda
