Home Kitaifa TASAF AWAMU YA III YAJA, VIONGOZI ZINGATIENI VIGEZO VYA KUWAPATA WALENGWA KUEPUSHA...

TASAF AWAMU YA III YAJA, VIONGOZI ZINGATIENI VIGEZO VYA KUWAPATA WALENGWA KUEPUSHA MALALAMIKO YALIYOJITOKEZA AWAMU ZILIZOPITA -RIDHIWANI  

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Wananchi kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo,

Na. Veronica Mwafisi-Manispaa ya Tabora

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete amewataka Viongozi mkoani Tabora kuzingatia vigezo vya kuwapata walengwa wa Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini unaoratibiwa na Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF).

Mhe. Kikwete amesema moja ya jambo kubwa ambalo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amekuwa akilisisitiza ni kusaidia Watanzania walio wanyonge. “TASAF awamu zilizopita illishia mwaka jana mwezi wa 9 lakini kwa upendo wake amepambana kuhakikisha fedha zinapatikana ili kusaidia Watanzania hao kuepukana na umaskini,” Mhe. Kikwete ameongeza.

Akizungumza na Wananchi katika Manispaa ya Tabora tarehe 9 Julai, 2026, baada ya kuhitimisha ziara yake kwa siku ya leo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora ya kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo, Mhe. Ridhiwani amesema sio sawa fedha hizo zikatumika kinyume kwa kuwaingiza kwenye Mpango wa Kunusuru Kaya Maskini watu wasiostahili. “Niwaombe mliopewa dhamana ya kusimamia zoezi hili kutenda haki kwa kuwaweka walengwa stahiki,” Mhe. Kikwete ameongeza.

Amesema kuna baadhi ya maeneo yalilalamikiwa kwa kufanya mambo ya ajabu na kutowatendea haki walengwa katika fedha walizokuwa wakipewa, niwaombe sana, tunapoanza mpango unaokuja, nisingependa yale mapungufu yaliyojitokeza kipindi cha nyuma yajirudie.

Ametoa wito kwa Wananchi kushiriki katika mikutano ya kutambua walengwa ili wapatikane watu sahihi. “Wananchi nanyi kwa kuwa mnashiriki katika mikutano ya kuibua walengwa, mkisomewa majina ya walengwa kama kuna ambao wameachwa mseme ili waongezwe na kama wamewekwa wasiostahili pia mseme ili watolewe kwani mkikaa kimya ndio matokeo yake wanaingizwa wasiostahili na baadae kuleta malalamiko.” ameongeza

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akizungumza na Wananchi kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo,

Sehemu ya Wananchi katika Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo na Mjasiriamali wakati Waziri huyo alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akisalimiana na Wazee wa Manispaa ya Tabora wakati Waziri huyo alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na Wananchi wa Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza nao wakati wa ziara yake ya kikazi aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

Sehemu ya Wananchi katika Manispaa ya Tabora wakimsikiliza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete alipokuwa akizungumza kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo,

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mhe. Ridhiwani Kikwete akicheza nyimbo ya ukaribisho katika Manispaa ya Tabora alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Manispaa ya Tabora wakati wa ziara ya kikazi ya Waziri huyo aliyoifanya katika Halmashauri ya Wilaya ya Sikonge, Halmashauri ya Wilaya ya Tabora na Manispaa ya Tabora iliyolenga kukagua utekelezaji wa miradi ya maendeleo.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here
Captcha verification failed!
CAPTCHA user score failed. Please contact us!